Maaskofu, mapadri, watakiwa kuhamasisha waamini kushiriki Kongamano la Ekaristi Takatifu
MAjimbo ya
Kanda (metropolitani) ya Magharibi yaaswa kuhamasisha zaidi waamini wao kwa
namna ya pekee kwenye maandalizi ya Kongamano la nne la Ekaristi Takatifu
kitaifa litakofanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora.
Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora
Mhashamu Paul Ruzoka hivi karibuni katika kikao cha saba cha maandalizi ya
Kongamano hilo kilichohudhuriwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC)
Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye ni
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya.
Akizungumza katika kikao hicho Askofu Ruzoka amewaomba wajumbe
kutoka majimbo ya Tabora, Kahama, Kigoma na Mpanda kuwa mabalozi wa kuhamasisha
waamini juu ya tukio hilo muhimu litakatolofanykika 1-5 July mwaka huu.
Aidha amewakumbusha wajumbe kusali sala maalum katika majimbo yote ya Tanzania kuliombea Kongamano hilo. Vile vile ameagiza
Kurugezi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Tanzania ihakikishe kwamba vyombo
vya habari vya majimbo yote vinashirikishwa kikamilifu katika maandalizi na
Kongamano lenyewe.
Akitoa salamu za Baraza la Maaskofu Tanzania ,Askofu Mkuu Gervas
Nyaisonga amesema, “Baraza limeridhika na maandalizi ya Kongamano na likotayari
kutoa ushirikiano wa hali na mali hadi kufikia kilele cha maadhimisho.”
Pamoja na hayo amewataka wawakilishi wa majimbo ya Metropolitani
ya Magharibi kuhamasisha maandalizi na ushiriki kwenye kilele cha Kongamano.
Mada zinazotarajiwa kutolewa kwa washiriki ni; Ekaristi Takatifu
na Wahudumu katika historia ya Kanisa, Ekaristi Takatifu katika Maandiko
Matakatifu, Ekaristi Takatifu na Umisionari, Ufafanunuzi wa Nembo ya Ekaristi
na Mama Bikira Maria na Ekaristi Takatifu.
Aidha kamati ratibishi ya Ekaristi Takatifu ilioneshwa na
kuhimizwa kusambaza vitenge vya Kongamano ambavyo vimeandaliwa na Kurungenzi ya
Mawasiliano ya Baraza kwa waamini ili kuendelea kulitangaza kongamano kwa
waamini.
Ili kufanikisha Kongamano hilo kamati mbalimbali za maandalizi
zimekwisha undwa na kupewa majukumu yake.
Aidha Majimbo ya metropolitani ya Magharibi inaendelea na uandishi
wa kitabu cha historia ya Ukristo Kanda ya Magaribi, yaani Tabora, Kahama,
Kigoma, Mpanda.
Ambayo historia itahusisha majimbo yalikuwa sehemu ya
Metropolitani ya Magharibi.
Sambamba na maadalizi hayo kila jimbo la Metropolitani ya
Magharibi linaendelea kuratibu mashindano ya kwaya kuanzia ngazi ya kigango
mpaka jimbo, ili hapo baadaye kwaya zitakazokuwa zimeshinda katika ngazi ya
jimbo zitaletwa kushindana katika ngazi ya metropolitani.
Wakichangia gharama za ushiriki kwa kila muumini, iliamuliwa kila
mshiriki atachangia kiasi cha shilingi laki mbili tu za kitanzania , ikiwa ni
gharama ya malazi, usafiri wa ndani kuelekea kituo cha hija (Ifucha) na chakula
kwa siku zote tano.
Miongoni wa wageni walioshiriki kwenye mkutano huo ni Askofu
Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki Singida, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya
Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mh.Padri Chesco Msaga na Paroko wa
Parokia Makongolosi Pd.Gaspar Mwangoka.
Baada ya Mkutano wajumbe walipata fursa ya kutembelea kituo cha
Hija cha Jimbo Kuu Tabora kilicho chini
ya watakatifu Yohana Paul II na Terezia wa Calcuta –Ifucha na kuona maendelea
ya ujenzi ikiwa na mahali ambapo kilele cha madhimisho ya Kongamano la Ekaristi
kitafanyika.
Comments
Post a Comment