Afya ya Baba Mtakatifu Fransisko inaimarika
DR.
Matteo Bruni Msemaji Mkuu wa Vatikani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
amebainisha kwamba, afya ya Baba Mtakatifu Fransisko ambaye hivi karibuni alikumbwa na mafua
makali inaimarika.
Hivi karibuni Papa Fransisko alikumbwa na mafua makali ambayo
yalimsababisha ashindwe kuhudhuria Mafungo ya Kwaresima 2020 kwa wasaidizi wa
karibu wa Baba Mtakatifu, “Curia Romana” kuanzia Machi 1- 6 mwaka 2020 huko
Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma.
Kwa sasa Papa Fransisko anaendelea pia kuadhimisha Ibada ya Misa
Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatikani.
Baba Mtakatifu pia anaendelea kufuatilia tafakari za mafungo ya
Kwaresima zinazotolewa kwa wafanyakazi wa “Curia Romana” huko Ariccia, nje
kidogo ya mji wa Roma.
Dr. Matteo Bruni amefafanua kwamba, Baba Mtakatifu anasumbuliwa na
mafua ambayo hayana uhusiano wowote na magonjwa mengine.
Tafakari wakati wa mafungo inaongozwa na Padri Pietro Enrico
Bovati, SJ, Katibu Mkuu wa Tume ya Kipapa ya Biblia na Mtaalam wa Sayansi ya
Maandiko Mtakatifu.
Kauli mbiu ya mafungo hayo ni “Kile kijiti kiliwaka moto: mkutano
kati ya Mwenyezi Mungu na binadamu mintarafu mwanga wa Kitabu cha Kutoka,
Injili ya Mathayo na Sala ya Zaburi.”
Comments
Post a Comment