Uchaguzi Mkuu kuangukia Jumatano imejibu maombi ya Wakristo – TEC
KATIBU Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania (TEC) Padri Charles Kitima, ameielezea hatua ya Serikali kuitangaza
Oktoba 28 kuwa tarehe ya kuppiga kura katika Uchaguzi Mkuu nchini, kwamba imietimiza ombi la muda mrefu la
waamini Wakkristo kufuatai tarehe hiyo kuangukia Jumatano ambayo siyo siku ya
Kiibada kwao.
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari,
katika mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake Kurasini jijini Dar es Salaam,
ambapo alisema tofauti na chaguzi zilizopita ambazo zimekuwa zikifanyika siku
ya Jumapili, uchaguzi wa mwaka huu umetekeleza kwa vitendo haki ya kila
Mtazania kuwa na Uhuru wa kuabudu na uhuru wa kupiga kura.
“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ibara ya 5 inaweka wazi haki ya kila Mtazania mwenye sifa zinazotakiwa
kushiriki kikamilifu uchaguzi iwe ni kwa kupiga kura au kuchaguliwa huku Ibara
ya nane pamoja na mambo mengine, inatoa uhuru wa kujitawala…hivyo uchaguzi wa
namna hii kufanyika Jumapili ulikuwa unagonganisha haki msingi za kuabudu na
kupiga kura,”
Hata hivyo alipendekeza uamuzi huu huwe
endeleavu yaani kwa tarehe ya uchaguzi kuangukia siku ambazo si za Ibada kwa
dini na madhehebu yote nchini.
“Leo tusifurahie Wakristo alafu uchaguzi
mwingine ukaangukia kwenye siku ambayo wenzetu Waislamu ama Wasababto
wanaitumia kuabudu, badala yake tunaomba liwe zoezi endelevu ya kuheshimu siku
hizo za kuabudu kwa imani zote,” amesisitiza.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeitangaza
Oktoba 28 mwaka huu kuwa siku ya kupiga kura kuwachagua rais, wabunge na
madiwani, ikiwa ni Uchaguzi Mkuu wa sita tangu Tanzania iingie kwenye Mfumo wa
vyama vingi nchini.
Hata hivyo hii itakuwa ni sehemu ya
historia kwani katika chaguzi kadhaa zilizopita, uchaguzi wa mna hiii umekuwa
ukifanyika siku ya Jumapili ambayo ni siku ya Kiibada kwa waamini wa Dini ya
Kikristo husuani wale ambao wapo chini ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
(TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) huku madhebu ya Kisabato yakisali
siku ya Jumamosi na upande wa Waislamu wao siku ya ya Ibada ni Ijumaa.
Miongoni mwa chaguzi hizo zilizofanyika
Jumapili kwa miaka ya hivi karibuni ni Uchaguzi Mkuu wa 2005 uliofanyika
Desemba 4 mwaka huo ambao hata hivyo ulikuwa ufanyike Jumapilipi ya Oktoba 3 mwaka
huo lakini ukahairishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Omar
Alli Juma. Mwingine ule wa mwaka 2015 uliofanyikaa Jumapili ya Oktoba 25 mwaka
huo.
Comments
Post a Comment