CCBRT yazidi kuwatia moyo wenye fistula
LICHA ya uhamasishaji unaofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulika na masuala ya afya la CCBRT,kuwahamasiha akinamama wenye tatizo la kutoka haja ndogo au kubwa bila kujitambua (Fistula)kujitokeza kupata matibabu bure ya ugonjwa huo, idadi inayojitokeza ni ndogo ikilinganishwa na hali halisi. Afisa Uhusiano wa CCBRT Bw. Abdul Kajumulo ameyasema hayo mwanzoni mwa juma wakati akizungumza na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kusimamiwa na Kanisa Katoliki nchini,mazungumuzo yaliyofanyika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) jijini Dar es Salaam. Amesema takribani watu 3,000 nchini Tanzania hukabiliwa na ugonjwa wa fistula kila mwaka, lakini kati ya hao ni wagonjwa 1,500 - 2,000 wanafika hospitali kwa ajili ya kupata tiba huku idadi iliyosalia wakiendelea kujificha majumbani, jambo lililoelezewa kukwamisha juhudi za kupunguza kasi ya zatizo hilo. Amezitaja baadhi ya sababu zinazochangia w...