Jubilei miaka 75 Masista wa Upendo
‘Mkiushinda ubinafsi mtafanikiwa’ Na Pascal Mwanache, Mbingu MASISTA wa Shirika la Upendo wa Mt. Fransisko Mahenge wameaswa kufanya kazi kwa kushirikiana huku wakiweka kando ubinafsi ili kazi zao ziendelee kumtukuza Mungu. Hayo yameelezwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Tundu-Masasi Mhashamu Filbert Mhasi katika Misa Takatifu ya kuwakumbuka marehemu waanzilishi wa shirika hilo la masista pamoja na masista waliofariki, ikiwa ni sehemu ya sherehe ya jubilei ya miaka 75 ya shirika la masista wa upendo wa Mt. Fransisko Mahenge. Akitoa homilia katika misa hiyo Askofu Mhasi amewaasa masista hao kutotafuta mtetezi mwingine zaidi ya Mungu pale wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali katika utume wao, bali wadumu katika uthabiti wa imani yao na Mungu atawatetea. “Inatupasa kumshukuru Mungu kwa imani tuliyojaliwa kupitia Kristo. Waanzilishi wa shirika hili walipigana vita vizuri na waliamini kuwa kuna maisha baada ya kifo. Ndiyo maana wakawa imara katika imani yao. Hawakuwa wabinaf...