Papa: Tunafanyia uchunguzi kashfa ndani ya Kanisa
BAba Mtakatifu Francisko katika mahojiano maalum na Kituo cha Televisheni cha Taifa nchini Mexico hivi karibuni pamoja na mambo mengine amezungumzia mauaji ya wanawake ndani ya familia, ukarimu kwa wakimbizi na wahamiaji; uhusiano kati ya siasa na uchumi; madhara ya biashara na matumizi haramu ya dawa za kulevya pamoja na kashfa ya nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo. Hii ni sehemu ya tafakari ya kina kuhusu hali halisi ya kimataifa sanjari na maisha na utume wa Kanisa kadiri anavyoufahamu Baba Mtakatifu Fransisko. Kuhusu shutuma za kashfa mbali mbali zinazoendelea kujitokeza ndani ya Kanisa, Baba Mtakatifu amesema kuwa, wanazifanyia kazi na kwamba, si kila kitu lazima kitolewe hadharani. Lazima uchunguzi ufanyike na kujiridhisha. Pia Kanisa lina nidhamu ya kuendesha kashfa na kwamba halifanyii kazi story za mitandao na maneno ya kuambiwa. Lazima lifanye uchunguzi wa kina. Jambo la msingi ni watu kuwa na uvumilivu, ili kutoa nafasi kwa viongozi wa Kanisa kufanya uchun...