Ukuaji uchumi usioheshimu mazingira ni uasi-Ask. Banzi
Na Pascal Mwanache, Korogwe I MEELEZWA kuwa uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa jina la maendeleo na ukuaji wa uchumi ni uasi sawa na kuabudu miungu, huku wito ukitolewa kwa kila mwanadamu kusheshimu kazi ya uumbaji. Hayo yamesemwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga Mhashamu Antony Banzi katika Misa Takatifu ya kuwasimika viongozi wapya wa Shirika la Masista wa mama yetu wa Usambara (COLU) iliyofanyika katika Makao Makuu ya shirika hilo huko Kwamndolwa, Korogwe. Akitoa homilia yake katika misa hiyo Askofu Banzi amesema kuwa mwanadamu amepewa mamlaka juu ya mazingira huku akitakiwa kutumia zawadi ya akili na utashi katika kuutiisha ulimwengu na vilivyomo kwa manufaa ya leo na kesho. “Kuiheshimu dunia ni moja ya maadili na ni amri ya Mungu. Kuharibu mazingira ni kuabudu miungu. Tusiitumie dunia kwa fujo kwani atakayeathirika ni mwanadamu mwenyewe. Tukiitunza nayo itatutunza” amesema Askofu Banzi. Pia ametaka kuwepo kwa njia rafiki katika uvuvi na ufugaji wa nyuki, huku ...