VAZI RASMI LA JUBILEI MIAKA 150 YA UKRISTO


Kamera yetu imewanasa baadhi ya waamini wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Kanisa Kigurunyembe, Jimbo Katoliki Morogoro wakiwa wamevalia nguo za kitenge ambacho ndilo vazi rasmi katika kuadhimisha Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara, ambapo kilele chake kitakuwa Novemba 4, 2018 kule Bagamoyo.

Hakika mama zetu hawa wamelitendea haki vazi hilo na hasa kwa mitindo mbalimbali waliyoshona kama inavyoonekana pichani. Unasubiri nini kujipatia kitenge hicho kwa ajili ya familia yako? Kinapatikana Kurugenzi ya Mawasiliano Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini jijini Dar es salaam. Weka oda yako kwa kupiga 0657835343.









Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI