Padri Makunde Katibu Mkuu mpya wa AMECEA
Maaskofu wanaounda Shirikisho la Mabaraza ya
Maaskofu Katoliki nchi za Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) wamemteua Padri
Antoni Makunde wa Jimbo Katoliki la Mbeya kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirikisho
hilo.
Uteuzi huo umekuja kufuatia uchaguzi uliofanyika
katika kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa 19 wa AMECEA Agusti 21, 2018 Addis Ababa.
Uteuzi
huo umetangazwa na Mwenyekiti wa AMECEA anayemaliza muda wake Mwadhama
Berhaneyesus Kardinali Souraphiel, Askofu Mkuu
wa Addis Ababa katika misa ya kufungwa kwa mkutano huo.
Padri
Makunde anachukua nafasi kutoka kwa Padri Ferdinand Lugonzo wa Jimbo Katoliki
Kakamega
nchini Kenya aliyehudumu kwa vipindi viwili katika nafasi hiyo.
Aidha
Mwadhama Berhaneyesus ametangaza uteuzi wa Padri
Stephen Mbugua, kutoka Jimbo Katoliki Nakuru nchini Kenya kuwa Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Kikatoliki Cha Afrika Mashariki– CUEA.
Padri
Mbugua anachukua nafasi ya Justus Mbae, kutoka Kenya ambaye amemaliza kipindi
chake cha kutumikia kama Makamu Mkuu wa Chuo.
Congratulation Father Makunde
ReplyDelete