Posts

Askofu Kinyaiya awataka waamini kuwaombea viongozi wa dini

Image
ASkofu Mkuu   wa Jimbo   Kuu   Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya amewataka   waamini na wote wenye mapenzi mema kuwaombea mapadri na watawa ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo. Wito huo hivi karibuni kwenye Misa ya kubariki mafuta ya wagonjwa, wakatekumeni na kuweka wakfu mafuta Matakatifu ya Krisma, katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma. Askofu Kinyaiya amesema kuwa mapadri ambao ndio wapakwa mafuta matakatifu wanapaswa kutambua kuwa wao ndio wateule wa Bwana wanaofanya kazi maalumu ya kutoa huduma katika Kanisa Mahalia. ‘’Ndugu zanguni mapadri na watawa nyie ndio mliopewa jukumu la kuwahudumia wana wa Mungu katika Kanisa hivyo mnapaswa kutenda yaliyo mema na ya kuwapendeza waamini mahali. Katu msifanye kazi ya Kanisa kwa ubaguzi. Tendeni kwa haki kwa kila mmoja atakayehitaji huduma ya kiroho,” amesema Askofu Kinyaiya. Pia akizungumzia jinsi Mafuta Matakatifu ya Krisma yanavyochanganywa kuwa mafuta Matakatif...

Maaskofu, mapadri, watakiwa kuhamasisha waamini kushiriki Kongamano la Ekaristi Takatifu

Image
MAjimbo ya Kanda (metropolitani) ya Magharibi yaaswa kuhamasisha zaidi waamini wao kwa namna ya pekee kwenye maandalizi ya Kongamano la nne la Ekaristi Takatifu kitaifa litakofanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora. Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhashamu Paul Ruzoka hivi karibuni katika kikao cha saba cha maandalizi ya Kongamano hilo kilichohudhuriwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye   ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki   Mbeya. Akizungumza katika kikao hicho Askofu Ruzoka amewaomba wajumbe kutoka majimbo ya Tabora, Kahama, Kigoma na Mpanda kuwa mabalozi wa kuhamasisha waamini juu ya tukio hilo muhimu litakatolofanykika 1-5 July mwaka huu. Aidha amewakumbusha wajumbe kusali sala maalum katika majimbo   yote ya Tanzania   kuliombea Kongamano hilo. Vile vile ameagiza Kurugezi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Tanzania ihakikishe kwamba vyombo vya habari vya majimbo yote vinas...

Afya ya Baba Mtakatifu Fransisko inaimarika

Image
DR . Matteo Bruni Msemaji Mkuu wa Vatikani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amebainisha kwamba, afya ya Baba Mtakatifu Fransisko   ambaye hivi karibuni alikumbwa na mafua makali inaimarika. Hivi karibuni Papa Fransisko alikumbwa na mafua makali ambayo yalimsababisha ashindwe kuhudhuria Mafungo ya Kwaresima 2020 kwa wasaidizi wa karibu wa Baba Mtakatifu, “Curia Romana” kuanzia Machi 1- 6 mwaka 2020 huko Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma. Kwa sasa Papa Fransisko anaendelea pia kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatikani. Baba Mtakatifu pia anaendelea kufuatilia tafakari za mafungo ya Kwaresima zinazotolewa kwa wafanyakazi wa “Curia Romana” huko Ariccia, nje kidogo ya mji wa Roma. Dr. Matteo Bruni amefafanua kwamba, Baba Mtakatifu anasumbuliwa na mafua ambayo hayana uhusiano wowote na magonjwa mengine. Tafakari wakati wa mafungo inaongozwa na Padri Pietro Enrico Bovati, SJ, Katibu Mkuu wa Tume ya Kipapa ya Bi...