Maaskofu Katoliki Tanzania wapewa mafunzo juu ya Uongozi Bora
Na Sarah Pelaji, Dar es Salaam B araza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa ushirikiano na Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki AMECEA na Missio, wametoa mafunzo kwa Maaskofu wa Kanisa Katoliki juu ya uongozi Bora. Mafunzo hayo ya siku tano yamefanyika kuanzia Januari 14-19, mwaka huu katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Kurasini jijini Dar es Salaam. Maaskofu hao wanajengewa uwezo juu ya Uongozi na Usimamizi wa taasisi, Uongozi Endelevu; Umoja wa Kanisa Katoliki pamoja na Ushauri na Usimamizi. Awali Katibu Mkuu wa AMECEA Padri Anthony Makunde ameeleza kuwa, mafunzo hayo ni ya awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza yalikuwa yanafadhiliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani sasa awamu ya pili yanafadhiliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani kupitia shirika lao la Missio. Aidha ameeleza kuwa alifanya safari na Rais wa AMECEA Mhashamu Charles Kasonde kwenda kukutana na Rais wa Missio Aach...