Askofu Chengula: Padri bora hanywi pombe kilabuni
Na Izack Mwacha, Mbeya WITO umetolewa kwa viongozi wote wa kiroho hususani mapadri kutambua kuwa kunywa pombe kilabuni siyo tabia za padri mzuri ambaye anamuwakilisha Kristo Duniani. Wito huo umetolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki Mbeya Mhashamu Evaristo Chengula wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Daraja ya upadri kwa Shemasi Jacob Machibya, iliyofanyika Parokia ya Chunya Jimboni Humo. Katika homilia yake Askofu Chengula amebainisha kuwa yapo mambo mengi ambayo yanawezesha kujua kiongozi bora na muadilifu mbele za watu, lakini kipimo ambacho pia kitaimarisha zaidi nafasi ya kiongozi kama padri muwakilishi wa Kristo ni pamoja na kufanya mambo sahihi na kwa wakati. “Sidhani kama litakuwa jambo la busara kwa padri kukaa kilabuni na kuanza kunywa pombe, hapana hiyo siyo tabia njema” amesisitiza Askofu chengula. Katika hatua nyingine Askofu Chengula amewaasa viongozi wa Halmashauri Walei kuwa na uwezo wa kuzungumza na mapadri wao bila ya kuwa na wasiwasi na jambo lolot...