Posts

Chaguo La Mhariri

Askofu Lebulu aadhimisha Jubilei ya Dhahabu ya Upadri

Image
  Na Sarah Pelaji, Same-Kisangara Juu A skofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha Mhashamu Josaphat Lebulu ameadhimisha Jubilei ya dhahabu ya   Upadri   yaani miaka 50 tangu alipopata Daraja Takatifu la Upadri. Jubilei hiyo imeadhimishwa Desemba 11 mwaka huu katika Parokia ya Kisangara Juu Jimbo Katoliki Same ambapo parokia hiyo pia imeadhimisha miaka 50 tangu ilipoanzishwa na katika parokia hiyo ndipo Askofu Mkuu Mstaafu Lebulu alipewa Daraja Takatifu la Upadri na   Askofu Joseph Kilasara Desemba 11 mwaka 1968. Katika maadhimisho hayo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Gervas Nyaisonga amesema kuwa, kwa niaba ya Maaskofu wakatoliki Tanzania, anampongeza Askofu Lebulu kwa kufanya kazi ya utume uliotukuka huku akimsihi aendelee kulisaidia Kanisa akitumia hekima na vipawa alivyojaliwa. “Ni wazi Askofu Lebulu amestaafu na anaadhimisha jubilei hii ya dhahabu lakini bado ana nguvu na anahitajika katika Kanisa. Sisi tunamuombea Mungu azidi kumpa ng

Uchaguzi Mkuu kuangukia Jumatano imejibu maombi ya Wakristo – TEC

Image
KATIBU Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Charles Kitima, ameielezea hatua ya Serikali kuitangaza Oktoba 28 kuwa tarehe ya kuppiga kura katika Uchaguzi Mkuu nchini,   kwamba imietimiza ombi la muda mrefu la waamini Wakkristo kufuatai tarehe hiyo kuangukia Jumatano ambayo siyo siku ya Kiibada kwao. Alitoa kauli hiyo   wakati akizungumza na vyombo vya habari, katika mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake Kurasini jijini Dar es Salaam, ambapo alisema tofauti na chaguzi zilizopita ambazo zimekuwa zikifanyika siku ya Jumapili, uchaguzi wa mwaka huu umetekeleza kwa vitendo haki ya kila Mtazania kuwa na Uhuru wa kuabudu na uhuru wa kupiga kura. “Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 5 inaweka wazi haki ya kila Mtazania mwenye sifa zinazotakiwa kushiriki kikamilifu uchaguzi iwe ni kwa kupiga kura au kuchaguliwa huku Ibara ya nane pamoja na mambo mengine, inatoa uhuru wa kujitawala…hivyo uchaguzi wa namna hii kufanyika Jumapili ulikuwa unagonganisha

Kahama Waanza Maandalizi Kumpokea Askofu Mpya

Image
Msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki Kahama Askofu Ludovick Minde ALCP/OSS amewataka mapadre,watawa na waamini kuendelea kusali na kudumisha umoja na mshikamano wanaposubiri mungu aweze kuwapatia Askofu mpya. Askofu Minde ambaye ni Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi amesema hayo katika misa takatifu iliytofanyika katika kanisa la Mtakatifu Karoli Lwanga iliyoambatana na kuzindua rasmi kamati ya maandalizi ya kumpokea rasmi Askofu Mpya anayekuja. Askofu Minde amewataka wanajimbo la Kahamaa kwa imani kuendelea kusali na kumuomba mungu aweze kuwapatia mchungaji mkuu wa jimbo hilo.

Kahama Waanza Maandalizi Kumpokea Askofu Mpya

Image
Msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki Kahama Askofu Ludovick Minde ALCP/OSS amewataka mapadre,watawa na waamini kuendelea kusali na kudumisha umoja na mshikamano wanaposubiri mungu aweze kuwapatia Askofu mpya. Askofu Minde ambaye ni Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi amesema hayo katika misa takatifu iliytofanyika katika kanisa la Mtakatifu Karoli Lwanga iliyoambatana na kuzindua rasmi kamati ya maandalizi ya kumpokea rasmi Askofu Mpya anayekuja. Askofu Minde amewataka wanajimbo la Kahamaa kwa imani kuendelea kusali na kumuomba mungu aweze kuwapatia mchungaji mkuu wa jimbo hilo.

Prof Makubi: Corona bado ipo wananchi msibweteke

Image
MGanga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amewataka   wananchi waendelee kuchukua tahadhari   juu ya maambukizi ya ugonjwa wa covi 19 unaosababishwa na virusi vya corona. Prof. Makubi ameeleza hayo   hivi karibuni alipokuwa anazungumza na   Gazeti Kiongozi kuhusu kile kinachosadikiwa na jamii kuwa tayari kuna dawa ya corona. “Ninachiotaka kuwaambia wananchi ni kwamba, hakuna dawa ya corona. Mpaka sasa dawa haijapatikana nna ile tuliyoleta kutoka Madagascar bado inafanyiwa uchunguzi kujiridhisha. Wananchi hawa vijana na wale waishio vijijini wanapaswa waelewe kuwa,   virusi vya corona havibagui umri wala mahali. Vijijini corona ipo tena ni rahisi kusambaa hasa kwenye minada na magulio. Hivyo waendelee kuchukua tahadhari kama zinavyoelekezwa   na serikali pamoja na wataalamu wa afya   ikiwemo WHO. Amewataka wenyeviti wa Mitaa, Vijiji, kata nk. kuweka mikakati ambayo itawasababisha wananchi   waendelee na shughuli zao za kiuchumi.   “Kwa mfano minada inaweza kuongezwa kwen

Vyombo vya Kanisa vyatakiwa kuzipa kipaumbele habari za Covid-19

Image
KATIKA kukabilianana Covid-19, vyomba vya habari vinavyomilikiwa na Kanisa Katoliki, vimetakiwa kuzipa kipaumbele habari zinazohusiana na mapambano dhidi ya virusi vya corona husani zile zinazotia matumaini, kuondoa hofu na woga kwa wananchi. Rai hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Mhashamu Flavian Kasala, katika mahojiano Maalum na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Baraza hilo, yaliyofanyika katikati ya juma jijini Dodoma. Askofu Kasala amehimza vyombo hivyo kutumia hata lugha za asili pale inapobidi ili kuhakikisha ujumbe unaeleweka kwa makundi yote ndani ya jamii. “Ni kweli lazima tuwe na mashaka, lakini mashaka haya yanatakiwa kuwa yenye matumaini…kumbe vyombo vyetu virudishe hayo matumaini kwamba binadamu anaweza kupigana vita na kushinda na hili ndilo wazo letu kubwa,” amesema. Pia ametoa wito kwa vyombo hivyo vya habari, kuhakikisha vinautumia ulivyo ujumbe wa TEC kuhusu ugonjwa huo wa Corona hasa kwa kuendana na mazingira halisi ya