Tabora kuenzi ndoto za Padri Nyamiti kuanzisha chuo cha muziki

KUFUATIA kifo cha Padri Prof. Charles Nyamiti kilichotokea Mei 19, 2020 katika Hospitali ya Mt. Anna Ipuli, Jimbo Kuu Katoliki Tabora limedhamiria kuendeleza ndoto za mtaalamu huyo wa muziki hasa za kuanzisha chuo cha muziki. Akizungumza na KIONGOZI mapema wiki hii Mratibu wa Idara ya Liturujia, Jimbo Kuu Katoliki Tabora ambaye pia ni mwanafunzi wa muziki wa Padri Nyamiti, Padri Deogratius Mwageni, amesema kuwa Padri Nyamiti alikuwa anatamani kuanzisha chuo cha muziki na yeye mwenyewe alikubali kujitoa ili aweze kufudisha nadharia ya muziki na vitendo. “Kwa kuanzia alikuwa na wanafunzi watatu ambao ni waseminari walioko likizo na mpaka siku ya mwisho kabla ya kifo chake alikuwa anafundisha muziki. Siku hiyo ya Jumatatu alifundisha kwa muda mrefu tena bila kuchoka mpaka alipoombwa apumzike. Ndipo akaenda kupumzika kidogo na akiwa mapumzikoni hali yake ilibadilika hivyo akapelekwa hospitali na baada ya vipimo akakutwa ana malaria kali” ameeleza Padri Mwageni. Ameongeza kuwa alil...