Utume wa Redio Maria Tanzania watua rasmi jimboni Musoma
ASkofu wa Jimbo Katoliki Musoma Michael Msonganzila, ameushukuru
uongozi wa Redio Maria Tanzania kwa kufika Jimboni Musoma kurusha matangazo
,kwani ilikuwa ni kiu ya waamini wa Jimbo hilo kufikiwa na Utume huo kwa miaka
mingi.
Akizungumza
wakati kukabidhiwa barua rasmi ya kutambulisha utume huo na Mhamsishaji Mkuu wa Redio Maria Tanzania
Emma Mahengo katika Jimbo hilo,Askofu huyo amesema kuwa ni zaidi ya miaka tisa
waamini wakisubiri kwa hamu kubwa kufikiwa na Utume huo.
“Imechukua
miaka 8 hadi 9 tangu tuombe utume huu wa Redio Maria Tanzania katika jimbo
letu.
Leo hii Machi 30 ,2020 tumepokea barua rasmi ya
kutambulisha utume huo kuanza hapa
kwetu. Binafsi ns kwa niaba ya waamini nimefurahi sana kwa hatua hii ,na hata
waamini wangu wamefurahi sana ,tuombe Mungu Mipango yote iende kama
ilivyopangwa ndani ya mwaka huu,”amesema Askofu Msonganzila.
Mwakilishi Kiongozi wa Redio Maria Kanda ya
Ziwa Stanslaus Mhema amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kurusha matangazo nchi
nzima na Jimbo la Musoma ni mojawapo ,hivyo waamini wawe tayari kuipokea redio
hiyo na kushirikiana katika kuiwezesha ili iendelee kufanya Utume wake.
Maparoko
walioshiriki Misa Takatifu iliyorushwa
live na Redio Maria jimboni humo,Paroko wa Parokia ya Kigera Padri Robert
Luvakubandi,Paroko wa Musoma Mjini Padri Benedict Luzangi,Paroko wa Parokia ya
Mwisenge Padri Valence Matungwa na Paroko wa Parokia ya Rwamlimi ,pamoja na
masista wa Moyo safi wa Afrika wa Jipe Moyo
wameishukuru timu ya redio kwa ,kufika katika parokia hizo na kurusha
matangazo yao moja kwa moja.
Comments
Post a Comment