Uchaguzi Mkuu kuangukia Jumatano imejibu maombi ya Wakristo – TEC
KATIBU Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Charles Kitima, ameielezea hatua ya Serikali kuitangaza Oktoba 28 kuwa tarehe ya kuppiga kura katika Uchaguzi Mkuu nchini, kwamba imietimiza ombi la muda mrefu la waamini Wakkristo kufuatai tarehe hiyo kuangukia Jumatano ambayo siyo siku ya Kiibada kwao. Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari, katika mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake Kurasini jijini Dar es Salaam, ambapo alisema tofauti na chaguzi zilizopita ambazo zimekuwa zikifanyika siku ya Jumapili, uchaguzi wa mwaka huu umetekeleza kwa vitendo haki ya kila Mtazania kuwa na Uhuru wa kuabudu na uhuru wa kupiga kura. “Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 5 inaweka wazi haki ya kila Mtazania mwenye sifa zinazotakiwa kushiriki kikamilifu uchaguzi iwe ni kwa kupiga kura au kuchaguliwa huku Ibara ya nane pamoja na mambo mengine, inatoa uhuru wa kujitawala…hivyo uchaguzi wa namna hii kufanyika Jumapili ulikuwa unago...