UJUMBE WA BABA MTAKATIFU KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA WAGONJWA DUNIANI FEBRUARI 11, 2019
“MLIPOKEA BILA
MALIPO, TOENI BILA MALIPO” (MT.10:8)
Wapendwa Kaka na dada zangu,
“Mlipokea bila malipo, toeni bila malipo”(Mt
10:8). Hayo ni maneno yaliyotamkwa na Yesu Kristu alipowatuma mitume wake
kwenda kueneza Injili,ili ufalme wake uweze kuenea kupitia matendo ya ukarimu
na upendo.
Mlipokea bila malipo, toeni bila malipo (Mt 10:8).
Katika kuadhimisha Siku ya Wagonjwa Duniani,
itakayoadhimishwa rasmi tarehe 11-2-2019 huko Calcutta, India, Kanisa- kama Mama
kwa watoto wake wote, na hasa walio wagonjwa, linatukumbusha kuwa ishara ya
ukarimu na upendo kama wa yule Msamaria Mwema kama njia thabiti ya
Uinjilishaji. Kuwajali na kuwatunza wajonjwa inahitaji utaalamu, upole, unyoofu
na unyenyekevu unaotolewa bila kujibakiza, matunzo yanayomfanya yule anaye
hudumiwa kuonja kupendwa.
Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu.Mt. Paulo
anauliza “ Ni kitu gani ulicho nacho ambacho hukupokea? (Kor. 4:7). Ni ukweli
na dhahiri kabisa kwa sababu ulicho na ulichonacho ni zawadi, maisha ya
mwanadamu hayawezi kufanywa kuwa ni mali binafsi ya mtu na hasa kwa sasa
kutokana na kukua kwa sayansi ya tiba na bioteknologia ambavyo vinaweza
kutushawishi kuchezea mti wa uhai (Mw 3:24).
Katika
utamaduni wa sasa wa kutapanya na kutojali, naomba nitamke kuwa “ukarimu”ndilo neno
lifaalo kutoa changamoto kwa tabia za sasa za ubinafsi na jamii kugawanyika;
ukarimu ukihuisha upya mahusiano mapya na ushirikiano kati ya watu na tamaduni
nyingine. Mazungumzano-ambayo ni chimbuko la ukarimu hufungua fursa ya
mwanadamu kukua na kuvunja utengano baina ya jamii. “Ukarimu” ni zaidi ya kutoa
zawadi inahusisha kujitoa binafsi, na siyo kuhamisha vitu au mali na kutoa kwa
wengine.
“Ukarimu”.
“Ukarimu”
hutofautiana na kutoa zawadi kwa sababu kutoa “zawadi” huhitaji kujitoa binafsi.
Ukarimu huchajizwa na nia ya kutaka kujenga uhusiano na yule anayepokea
ukarimu/zawadi. Ni hali ya kuwakubali wengine ambayo ndio msingi wa jamii. Ukarimu
ni asili ya Mungu, ukarimu wa Mungu ambao ulifikia kilele kwa ujio wa Mwanae na
kushuka kwa Roho Mtakatifu.
Kila mmoja wetu
ni maskini, mhitaji na fukara. Tunapozaliwa, tunahitaji matunzo toka kwa wazazi
ili tuishi, na katika kila hatua ya maisha tunabaki wategemezi kwa watu wengine
kwa kiwango fulani. Daima tunakuwa tunatambua kuhusu udhaifu wetu kama
“viumbe”, mbele ya watu wengine na dhaifu katika hali mbalimbalihali. Unyenyekevu
wa kukubali udhaifu wetu utufanye tuone haja ya kushirikiana na wengine kama
tendo la fadhila katika maisha.
Kuukubali ukweli huo hutufanya tutende kwa
kuwajibika kwa kukuza yaliyo mema kwa mtu binafsi na kwa jamii. Ni pale tu
tutakapojiona, sio kama tulio jitenga na dunia bali tulio katika maungano na
wengine, tutaweza kujenga utamaduni wa
umoja unaojali dunia yetu ya pamoja.
Tusiogope kujiona wahitaji au wategemezi kwa
wengine, kwa sababu binafsi na kwa juhudi zetu tuu hatutaweza kumaliza
mapungufu yetu. Kwa hiyo tusiogope kukiri mapungufu yetu,kwa kuwa Mungu
mwenyewe,kupitia Yesu Kristu alijinyenyekesha kwetu (Wafil. 2:8) na anaendelea
kufanya hivyo; na katika
umaskini/udhaifu wetu anatusaidia na kutukirimu zaidi ya matarajio yetu.
Katika kuadhimisha
rasmi siku hii nchini India, napenda kukumbusha kwa furaha na kuenzi mfano wa
Mt.Teresia wa Calcutta- ambaye ni mfano wa ukarimu uliodhihirisha upendo wa
Mungu kwa maskini na wagonjwa. Kama nilivyo sema wakati wa kutangazwa
mtakatifu, Mama Teresa, maisha yake yote yalikuwa ni ya kumimina/kusambaza huruma ya Mungu, akajiachia aweze kutumika
kwa ajili ya wote na kuwa mtetezi wa uhai wa wale ambao hawajazaliwa na wale
walioachwa na kutupwa. Alijinyenyekeza kwa walioachwa wafe kandokando mwa
barabara, akiona ndani mwao hadhi na uzuri wao wa Kimungu. Alifanya sauti yake
ikasikika miongoni mwa wenye mamlaka ya dunia wajitambue na wasutwe na dhamiri
zao kwa maovu--maovu na umaskini walio utengeneza kwa watu wengine.
Kwa Mama
Teresa, huruma ilikuwa chumvi iliyotoa ladha kwa kazi yake. Ilikuwa ni mwanga
ulioangaza kwenye giza la wengi ambao hawakuwa tena na machozi ya kulia
kutokana na umaskini na mateso. Utume wake katika miji na pembezoni mwa miji umebaki
kuwa ushuhuda wa ukaribu wa Mungu kwa maskini (Homily, 4 September 2016)
Mtakatifu, Mama
Teresa, tusaidie kuelewa kuwa kipimo cha matendo yetu kiwe upendo wa
kutojibakiza kwa kila mwanadamu, bila kujali lugha, kabila au dini ya mtu. Mfano
wake unaendelea kutuongoza kwa kufungua fursa za furaha na matumaini kwa wote
wenye kiu ya uelewa na upendo na hasa wale wanaoteseka.
Ukarimu huchochea
na kudumisha kazi nyingi za wahudumu wa kujitolea ambazo ni muhimu sana katika sekta ya afya na hasa matunzo ya
wagojnwa;wahudumu ambao wanawakwa na moyo wa msamaria mwema.
Nitoe shukrani
zangu na kutia moyo taasisi zote za wahudumu wa kujitolea waliojikita katika
kuwasafirisha na kuwasaidia wagonjwa, wale wote wanao hamasisha uchangiaji wa
damu na uchangiaji wa viungo vya kusaidia wengine. Huduma za kujitolea ni moja
ya eneo la pekee linalodhihirisha umuhimu wa Kanisa katika utunzaji wa wagonjwa
na utetezi wa haki za wagonjwa na hasa wale walio athiriwa na magonjwa
yanayohitaji uangalizi maalumu. Napenda pia kutambua juhudi kubwa mnayofanya ya
kujenga ufahamu na kuzuia magonjwa .Kazi yenu ya kujitolea katika vituo vya
afya na nyumbani pamoja na kutoa
uangalizi na kutoa huduma za kiroho ni ya umuhimu na msingi mkubwa.
Wagonjwa
wasiohesabika walio peke yao, wazee, waliodhaifu kiakili na kimwili wanafaidika
na huduma zenu. Nawahimiza kuendelea kuwa ishara ya uwepo wa Kanisa katika
dunia ya sasa. Mhudumu wa kujitolea ni rafiki mzuri ambaye mgonjwa anaweza
kueleza mawazo yake na hisia zake kutokana na uvumilivu na unyenyekevu wao wa
kusikiliza, voluntia anamwezesha mgojwa aache kuwa ni mpokea huduma bali
mshiriki mkamilifu wa mchakato wa matibabu hali inayo rudisha matumaini na
kufungua milango ya kuwa wazi ili kuboresha matibabu. Kazi ya voluntia hueneza
maadili mema, matendo mema na kujenga mfumo wa kuishi ulio jikita katika misingi
ya ukarimu. Ni njia nyingine ya kufanya huduma za afya ziwe ni za kibinadamu
zaidi.
Roho ya ukarimu inapaswa kuchochea taasisi za
afya za Kikatoliki iwe ziko katika nchi zilizoendelea au katika nchi maskini za
dunia yetu kwa kutoa huduma zao wakiongozwa na Injili.Taasisi za Afya za
Kikatoliki zinaalikwa kuwa mfano wa kujitoa, wa ukarimu na zenye mshikamano
kama mwitiko dhidi ya hulka ya kutaka faida bila kujali madhara; hulka ya kutoa
ili kupokea na hulka ya kunyonya bila huruma.
Nahimiza kila mmoja, katika ngazi zote kukuza
moyo wa ukarimu na wa kuwa zawadi kwa wengine kama njia pekee ya kushinda utamaduni
wa kutaka faida na utapanyaji. Taasisi za afya za Kanisa Katoliki zisitumbukie
katika mtego wa kuendesha bisashara ya huduma za afya, zinapaswa kujikita
katika kumhudumia mtu kuliko kuangalia faida.Tunatambua kuwa huduma za afya ni
shirikishi, inayohusu kufanyakazi na wengine, inayohitaji kuaminiana, urafiki
na mshikamano. Ni hazina inayofurahiwa kikamilifu pale inapotolewa kwa wengine.
Furaha ya kujitoa na kuwa zawadi kwa wengine ndiyo (barometer) kipimo cha afya
ya Mkristu.
Nawakabidhi
nyote kwa Maria mfariji wa wagonjwa. Atusaidie kushirikishana karama
tulizopokea kwa roho radhi ya masikilizano na kupokeana, tuishi kama kaka na
dada katika Kristu tukiwa makini kutambua mahitaji ya wengine, kutoa kwa moyo
wa ukarimu na kujifunza moyo wa kujitoa kwa ajili ya wengine.
Kwa upendo
mkuu,nawahakishia ukaribu wangu nanyi katika sala na kwenu nyote nawatumia baraka
za Kitume. Vatican City, 25 November 2018
Katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Kristu Mfalme wa Ulimwengu
FRANCIS - PAPA
Comments
Post a Comment