Askofu Rweyongeza: Wakatoliki msidanganywe na watenda miujiza
WAkristo wakatoliki wametakiwa kuwa na msimamo wa imani na kufuata kanuni na misingi ya Imani ya Kanisa Katoliki. Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo Katoliki Kayanga Mhashamu Almachius Vicent Rweyongeza katika misa Takatifu ya Kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 10 ya Jimbo la Kayanga na miaka 10 ya Uaskofu wake. Misa hiyo iliyoambatana na uzinduzi wa nyumba ya Kiaskofu Jimboni Kayanga. Amesema kuwa mkristo mkatoliki kamwe hatakiwi kuwafuata wanaokuja kuwadanganya na kuwalaghai kwa fedha, magari na mali za kupita hapa duniani . Mkristo anatakiwa kuwa na subira , uvumilivu pamoja na kuwa na imani thabiti ambayo itasaidia kung’oa visiki na milima na kufuata kanuni msingi za Kanisa Katoliki. Akofu Rweyongeza amesema kuwa ‘’Wahubiri feki huwahubiria watu tusiowafahamu,na wale wenye magonjwa sugu ambao tunawafahamu hawawafuati kuwaponya. Wanatuletea watu feki ambao wameandaliwa nanyi mnawafuata. wangekuwa waponyaji kw...