Naibu Waziri Kwandikwa atoa msaada katika shule ya Jimbo la kahama
Na Patrick Mabula, Kahama. NAIBU waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu , Wilaya Kahama amelishukuru Kanisa Katoliki kwa mchango wake katika kutoa huduma za jamii ikiwemo afya na elimu. Amesema hayo alipotembelea shule hiyo hivi karibuni katika ziara yake mjini Kahama ili kutekeleza ahadi yake aliyoitoa kwa shule hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya wahitumu wa darasa la saba mwaka 2016. Hivyo ameambatanisha shukrani hizo kwa kutoa msaada wa komputa mbili zenye thamani ya shilingi 2,000,000 katika shule ya msingi ya Mtakatifu Athony wa Padua ya jimbo Katoliki Kahama. “Serikali inatambua mchango wa Kanisa katika huduma za jamii. Nami ninawashukuru sana kwa kazi hiyo ya kuunga mkono jitihada za serikali. Nami ninaunga mkono jitihada zenu kwa kidogo nilichotoa ili kwa pamoja tulijenge taifa letu,” amesema. Kwa upande wao watoto wanaosoma shule ya hiyo ya Mtakatifu Athony w...