Posts

Padri Makunde Katibu Mkuu mpya wa AMECEA

Image
Maaskofu wanaounda Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki nchi za Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) wamemteua Padri Antoni Makunde wa Jimbo Katoliki la Mbeya kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirikisho hilo. Uteuzi huo umekuja kufuatia uchaguzi uliofanyika katika kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa 19 wa AMECEA Agusti 21, 2018   Addis Ababa. Uteuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa AMECEA anayemaliza muda wake Mwadhama   Berhaneyesus Kardinali Souraphiel, Askofu Mkuu wa Addis Ababa katika misa ya kufungwa kwa mkutano huo. Padri Makunde anachukua nafasi kutoka kwa Padri Ferdinand Lugonzo wa Jimbo Katoliki Kakamega nchini Kenya aliyehudumu kwa vipindi viwili katika nafasi hiyo. Aidha Mwadhama Berhaneyesus ametangaza uteuzi wa Padri Stephen Mbugua, kutoka Jimbo Katoliki Nakuru nchini Kenya kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Cha Afrika Mashariki– CUEA. Padri Mbugua anachukua nafasi ya Justus Mbae, kutok...

PAPA AMEMTEUA PADRI ANTHONY LAGWEN KUWA ASKOFU WA MBULU

Image
Mh. Pd. Anthony Lagwen ateuliwa kuwa Askofu Jimbo Katoliki la Mbulu Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Anthony Lagwen kutoka Jimbo Katoliki la Mbulu, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Mbulu, nchini Tanzania. Askofu mteule Anthony Lagwen alizaliwa tarehe 5 Julai 1967 huko Tlawi, Jimboni Mbulu. Baada ya masomo yake ya msingi, alibahatika kuendelea na masomo ya sekondari katika Seminari Ndogo ya Sanu, Jimbo Katoliki la Mbulu. Akapata masomo ya falsafa kutoka Seminari kuu ya Ntungamo, iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba na baadaye akahamia Seminari kuu ya Kipalapala, Jimbo kuu la Tabora ili kuendelea na masomo ya kitaalimungu. Tarehe 18 Oktoba 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki Mbulu. Tangu wakati huo, katika maisha na utume wake wa Kipadre kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000, alikuwa Paroko-usu wa Parokia ya Bashay. Kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2004 akepelekwa na Jimbo kujiendeleza zaidi katika masuala ya biashara kwenye Chuo Kikuu cha Mtaka...

Suluhu ya maadili kwa mapadri, wanandoa ni malezi kwa vijana

Image
Na Sarah Pelaji, Dar es Salaam A skofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian Kassala ameiasa jamii kuwekeza kwenye malezi kwa vijana ili kutatua changamoto zilizopo katika ndoa, upadri, utawa na katika nyanja zote za jamii. Akizungumza na Gazeti Kiongozi, Askofu Kassala amesema kuwa, ulimwengu wa sasa umegubikwa na changamoto mbalimbali kwasababu jamii inazembea malezi kwa watoto na vijana. “Miito mitakatifu ya Ndoa, Upadri, utawa inaitikiwa na watu ambao wapo tayari kuelekezwa, kutengenezwa na kulelewa ili wamudu maisha waliyoitiwa na Mungu. Upadri pamoja na kuwa ni wito bado unahitaji malezi, uelekezi na kumtengeneza kijana aweze kuwa padri anayehitajika katika jamii. Analelewa ili awe na tabia zenye utu ndani mwake , upendo, wema, uwajibikaji, uchaji wa Mungu nk. Seminari hazipokei watu wakamilifu, watu ambao tayari wameshatengenezwa (ready made) hapana ndiyo maana kuna muda wa malezi    ili kijana apate malezi ya kuweza kuuishi upadri wake. ...