Posts

KARDINALI PENGO APONGEZA JUHUDI ZA ASKOFU SANGU 

Image
n Na Joachim Mahona, Shinyanga. A SKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar-es-salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu za kulistawisha Jimbo na kutoa huduma mbalimbali za kijamii jimboni humo. Akizungumza mara baada ya kuongoza misa takatifu ya dominika ya kwanza ya majilio katika Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku nne aliyoifanya jimboni Shinyanga, Kardinali Pengo amebainisha kuwa amepata faraja kubwa baada ya kutembelea miradi mbalimbali na kuona jinsi Askofu Sangu anavyofanya juhudi kubwa za kulistawisha Jimbo kwa kushirikiana na mapadri na waamini kwa kipindi kifupi tu cha miaka miwili tangu aanze utume wake. “Narudi Dar-es-Salaam nikiwa naamini kuwa Jimbo hili limepiga hatua kubwa katika hali ya kushangaza, nilikuwa na wasiwasi wakati wa kumwekea mikono siku ile tuliyokuwa tukimweka wakfu kuwa Askofu wa Shin...

UISHINI UTAKATIFU KABLA YA KIFO-ASK MSONGANZILA

n Na Veronica Modest, Musoma A SKOFU wa Jimbo Katoliki Musoma Mhashamu Michael Msonganzila amewakumbusha waamini wa Kanisa hilo, kuhakikisha wanajiweka katika maisha ya Utakatifu kabla ya kufariki dunia kwa kuwa mchakato wa kutangazwa mtakatifu ni wa muda mrefu.  Askofu Msonganzila ameyasema hayo katika Misa Takatifu ya kuweka nadhiri za kwanza kwa masista 9 wa shirika la Moyo Safi wa Bikira Maria Afrika, jubilei ya miaka 25 kwa masista wawili na jubilei ya miaka 50 ya utawa kwa sista mmoja, Misa iliyofanyika katika Kanisa la Novisiati lililopo parokia ya Nyamiongo jimboni humo. Amesema kuwa waamini wengi wamekuwa wakisubiri kutangazwa watakatifu baada ya kufariki kitendo ambacho kimekuwa kikichukua muda mrefu, hivyo ni vyema kila mkristo akahakikisha anaishi maisha ya unyenyekevu, upendo, utii na usafi wa moyo kabla ya kusubiri mchakato wa kutangazwa kuwa mtakatifu.  Pia amewapongeza watawa wote kwa hatua yao ya utume ambapo amewaomba waliotimiza miaka 25 na 50 ku...

UTOAJI MIMBA, VIDHIBITI MIMBA TISHIO NCHINI

Image
n Na Pascal Mwanache, Dar I MEELEZWA kuwa utoaji wa mimba na matumizi ya vidhibiti mimba ni dhana zinazolenga kuharibu taifa na kushambulia maadili, utamaduni na imani ya taifa huku dhana hizo zikiwa ni itikadi ovu za magharibi za kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai nchini (Pro life) Emil Hagamu katika tathmini yake ambapo amesema kuwa utoaji wa mimba na matumizi ya vidhibiti mimba ni vitu vigeni kwa waafrika na ili vikubalike hutumika kampeni na propaganda yenye maneno mazuri ili kuficha uovu uliomo ndani yake. “Taifa lolote linaweza kuangamizwa njia ya vita. Vita kubwa tunayopigwa watanzania ni mashambulizi dhidi ya maadili ya Taifa ambayo ndiyo yanayotafsiri jamii ilivyo. Ukiua utamaduni unaojenga misingi ya maadili na imani utakua umeua taifa. Na ukitaka kuua vizuri Taifa basi lenga kwa vijana, ukibomoa misingi ya hawa lazima utamomonyoa taifa” Aidha amesema kuwa fikra za kuzaa, idadi ya watoto, na namna ya kupis...