Posts

MAHAKAMA YA MAFISADI RASMI JULAI

Image
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amebainisha kuwa sasa mahakama rasmi ya mafisadi itaanza kazi Julai mwaka huu. Akiongea mkoani Geita katika Misa Takatifu ya kumsimika na kumweka wakfu Askofu Flavian Kassala Jimbo la Geita hivi karibuni,waziri mkuu amesema sasa wote wanaoendekeza vitendo vya ufisadi kiama chao kimefika. Kassim Majaliwa amesikitika kuona mafisadi wanasababisha wananchi wasio na hatia kuteseka na wakati mwingine kupoteza maisha kutokana na mafisadi wachache wasio na huruma wala utu kutumia nafasi walizonazo kujinufaisha. Amesema kanisa limefanya jitihada kubwa kujenga jamii yenye amani,upendo na kuthamini utu lakini bado tatizo la ufisadi limeendelea. Amelipongeza kanisa na kuliomba liendelee kuipa serikali ushirikiano katika vita hiyo kama linavyofanya katika utoaji wa huduma za kijamii. Waziri mkuu Majaliwa licha ya kusema kanisa linaongoza nchini katika kutoa huduma za kijamii,amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili huduma hizo ziendelee kuinufa...

PAPA FRANCISKO AWAASA WANAHABARI

Image
Baba Mtakatifu Francisko anawataka wanahabari kuhakikisha kwamba, wanatekeleza kikamilifu dhamana hii kwani habari njema zinasaidia mchakato wa maendeleo ya watu: kiroho na kimwili. Baba Mtakatifu ameyasema haya, Jumapili tarehe 26 Juni 2016 alipokuwa anarejea kutoka katika hija yake ya kitume nchini Armenia. Akiwa njiani, Baba Mtakatifu aliweza kujibu maswali kumi kutoka kwa waandishi wa habari ambao wamekuwa kwenye msafara wake wakati wa hija yake ya kitume nchini Armenia kuanzia tarehe 24- 26 Juni 2016. Baba Mtakatifu amegusia urithi na ushupavu wa imani kwa familia ya Mungu nchini Armenia na kwamba vijana wanapaswa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa haki, amani na upatanisho nchini Armenia. Mauaji ya kimbari ni ukweli wa kihistoria usioweza kufumbiwa macho! Papa mstaafu Benedikto XVI ni mlinzi makini wa Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake. Sinodi ya Kanisa la Kiorthodox imekuwa na mafanikio makubwa ingawa mambo yanaweza kuboreshwa zaidi. Umoja wa...

MAGAZETI YAMEANDIKA HIKI LEO JUMANNE JUNE 28

Image

PAPA HANA SABABU YA KUANZISHA VITA VYA KIDINI

Image
Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anakiri kwamba, hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Armenia kuanzia tarehe 24- 26 Juni 2016 imekuwa na mafanikio makubwa na kwamba, ilijikita katika mambo makuu matatu: kwanza kabisa Baba Mtakatifu amepata fursa ya kuweza kukutana na kuzungumza na familia nchini Armenia na kwamba, wananchi wamefurahishwa sana na uwepo wa karibu wa Baba Mtakatifu katika maisha yao. Imekuwa ni nafasi ya kufanya rejea katika utajiri mkubwa unaofumbatwa katika historia ya wananchi wa Armenia na kwamba, sala ya kiekumene ni kati ya matukio makubwa yaliyogusa watu wengi wakati wa hija ya kitume ya Baba Mtakatifu nchini Armenia. Padre Lombardi anakaza kusema, dhana ya Uekumene, Ukarimu, Umoja na Udugu ni fadhila ambazo zimeshuhudiwa na Patriaki Karekin II katika kipindi cha siku tatu za uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko katika makazi yake. Kuna matukio makubwa yaliyopamba hija ya Baba Mtakatifu huko Armenia ambayo yataendelea ku...

ZIARA YA ARMENIA:TAMKO LA VIONGOZI WA MAKANISA

Image
Baba Mtakatifu Francisko na Patriaki Karekin II wa Kanisa la Kitume la Armenia Jumapili tarehe 26 Juni 2016, wametia sahihi kwenye Tamko la Pamoja kwa kumshukuru Mungu kutokana na uhusiano mwema wa imani na upendo unaoendelea kujengeka kati ya Makanisa haya mawili kama mashuhuda amini wa Injili ya wokovu inayopania kuleta faraja na matumaini katika ulimwengu mamboleo unaokabiliwa na kinzani nyingi. Viongozi hawa wanaimba utenzi wa sifa na shukrani kwa Fumbo la Utatu Mtakatifu kwa kutambua kwamba, Mwenyezi Mungu daima ataendelea kuwa msimamizi na wokovu wao. Kunako mwaka 2001, Kanisa la Kitume nchini Armenia wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 1700 tangu nchi hiyo ilipotangaza Ukristo kuwa ni dini rasmi ya Armenia, Mtakatifu Yohane Paulo II alitembelea Armenia, akawa ni shuhuda wa kurasa mpya za ushuhuda wa uhusiano wa kidugu kati ya Kanisa la Kitume la Armenia na Kanisa Katoliki. Wanamshukuru Mungu pia kwa kuwawezesha kunako tarehe 12 Aprili 2015, kushiriki...

UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA NA MABADILIKO UKUU WA MKOA HAYA HAPA..

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine. Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stansla...

MAGAZETINI LEO JUMATATU JUNE 27

Image