Posts

UZINDUZI WA MIAKA 20 YA REDIO MARIA WAFANA DAR ES SALAAM..

Image
Matukio mbalimbali ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 ya Uinjilishaji wa Radio Maria Tanzania tangu kuanzishwa kwake. Uzinduzi huo umefanyika katika Kanisa la Mt. Maxmilian Maria Kolbe Parokia ya Mwenge Jimbo Kuu Dar es Salaam. Uzinduzi huo umehudhuriwa na waamini kutoka ndani na nje ya Parokia ya Mwenge wakiwemo waanzilishi wa Redio hiyo hapa nchini, Marafiki pamoja na wadau mbalimbali. Adhimisho la Misa Takatifu lili ongozwa na Askofu wa Jimbo Mtwara Mhashamu Titus Mdoe akishirikiana na Paroko wa Parokia ya Mwenge na Msaidizi wake Padri Sixbert Heri, Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi Sinza Padri Cathibert Sasagu Maganga na Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padri John Maendeleo. Radio Maria ilianza kurusha matangazo yake nchini mwaka 1996 ambapo makao makuu yalikuwa Jimbo Kuu Songea na sasa makao makuu yapo Mikocheni Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Kilele cha maadhimisho haya k...

MAPAMBANO DHIDI YA NJAA..

Image
Utunzaji bora wa mazingira ni sehemu muhimu sana ya Mafundisho Jamii ya Kanisa, changamoto ya kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha utu na heshima ya binadamu; ustawi na mafao ya wengi kwa kujikita katika mshikamano unaoongozwa na kanuni auni. Binadamu anakumbushwa kwamba, amekabidhiwa kazi ya kulinda, kutunza na kuendeleza mazingira kwa ajili ya ustawi na mafao ya wengi, dhamana inayojikita katika haki.  Jumuiya ya Kimataifa haina budi kushikamana katika mapambano dhidi ya baa la njaa na utapiamlo kwa kuondokana na tabia ya uharibifu wa chakula ambacho kingeweza kuganga njaa sehemu mbali mbali za dunia. Sekta ya uchimbaji wa madini haina budi kuwanufaisha wananchi sanjari na kulinda mazingira kwa kutumia teknolojia rafiki, daima binadamu akipewa kipaumbele cha kwanza!  Kwa ufupi haya ndiyo mawazo makuu yaliyotolewa na Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la haki na amani, Jumatatu, tarehe 25 Aprili 2016 kwenye mkutano wa siku mbili ku...

KIPAIMARA:SERENGETI WAIMARISHWA

Image
ASKOFU wa Jimbo katoliki Musoma Michael Msonganzila ametoa sakramenti ya kipaimara kwa waamini wa Parokia ya Serengeti inayoongozwa na Padri Bernald Chegere,iliyopo ndani ya hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Serengeti,ikiwa ni sehemu ya kuwasogezea huduma ya kiroho wafanyakazi waliomo ndani ya hifadhi hiyo ambao ni vigumu kuifuata huduma hiyo mjini Mugumu. Pia Askofu Msonganzila ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la kanisa lililopo parokia ya Serengeti iliyopo ndani ya hifadhi hiyo ili kuifikisha haraka huduma ya kiroho kwa watumishi wa idara mbalimbali waliomo ndani ya hifadhi. Victoria Modest,Musoma

MAGAZETI LEO JUMATATU APRILI 25 YAMEANDIKA HIKI:KISOME

Image

INJILI YA AMANI KWANZA..

Image
Baraza la Kipapa la haki na amani kwa kushirikiana na Chama cha kitume cha “Pax Christi” hivi karibuni linaendesha mkutano wa kimataifa kuhusu Mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu vita na amani sanjari na kuachana na dhana ya “vita halali na ya haki”, ili kujenga na kudumisha kanuni maadili zinazolenga kukuza na kudumisha misingi ya haki na amani, ili kupambana na mauaji ya kimbari.  Wajumbe wa mkutano huu katika tamko lao wamekazia umuhimu wa Kanisa Katoliki kujikita zaidi na zaidi katika kukuza na kudumisha Injili ya amani mintarafu Maandiko Matakatifu. Mpango mkakati huu sasa unapaswa kufundishwa seminarini, kwenye taasisi za elimu ya juu na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki. Wajumbe wanasema, ulimwengu mamboleo unasheheni hofu na wasi wasi ya vita, athari za myumbo wa uchumi kimataifa, vita na mipasuko ya kijamii, changamoto kwa Wakristo kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Injili ya amani, ujumbe uliotangazwa na kushuhudiwa na Kristo Ye...