Posts

MAFUNGO YA PASAKA:WATAWA WASHIRIKI MUSOMA

Image
WATAWA wenye nadhiri za muda wa jimbo katoliki Musoma wameshiriki kwenye mafungo kwa ajili ya pasaka. Katika picha hizi anayeonekana akitoa neno la imani ni Padri John Bosco Kiyuga ambaye ni Paroko wa Parokia ya Nyamiongo Jimboni Musoma. Victoria Modest,Musoma

MAPADRI WAIELIMISHA JAMII MAANA YA IJUMAA KUU LUNINGANI.

Image
LEO asubuhi mapadri wanne,PAUL CHIWANGU,GERLAD KAMINA,STEPHANO KAOMBE,..,wameshiriki katika vipindi vya asubuhi luningani kuuelimisha umma nini maana ya siku ya ijumaa kuu,alhamisi,pasaka na mambo kadha wa kadha kuhusu kanisa katoliki. Jamii imeipokea elimu hiyo kwa furaha kubwa huku ikihamasika kushiriki katika safari ya mateso na hatimaye kufufuka kwa bwana Yesu Kristu. Blog hii inawashukuru sana TBC,STAR TV,CHANNEL TEN,ITV kwa kuliamini baraza la maaskofu katoliki Tanzania na kuwaalika mapadri hawa kuuelimisha umma. Pia blog hii inaendelea kuukumbusha umma kuwa NDICHO KISEMEO CHA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI.Hivyo kwa lolote lile lihusulo kanisa katoliki na hasa kwa wanahabari,utalipata humu. ASANTENI SANA.

BABA ASKOFU MSONGANZILA AOSHA MIGUU WAKAZI WA MUSOMA.

Image
Askofu wa jimbo katoliki Musoma Michael Msonganzila akiwaosha miguu waamini kutoka makundi  yote wakati wa ibada ya Alhamisi kuu katika kanisa kuu la Mtakatifu Mama Bikira Maria wa Mungu jimboni Musoma. Veronica Modest,Musoma

LUGHA MOJA

Image
PAPA FRANCIS AKIBUSU MIGUU YA WAHAMIAJI..

PAPA FRANCIS AOSHA MIGUU WAISLAMU,WAKRISTU,WABUDHA..

Image
Baba Mtakatifu Francis ameosha miguu ya wahamiaji 11 wakiwemo waislamu watatu,wakristu wanne,waorthodox,wahindu na volunteer mmoja mjini Rome katika tukio la unyenyekevu linaloambatana na itikadi ya kuanza kwa msimu wa Pasaka. Papa Francis alitembela makao ya wahamiaji, mjini Roma na kuendesha misa ya kuanza kwa msimu wa pasaka. Ziara yake katika kituo hicho cha kutathmini uhalali wa wahamiaji cha (Castelnuovo di Porto), inawadia huku uhasama na taharuki ikienea kote barani ulaya kuhusiana na kuwepo kwa wahamiaji hasa kufuatia mauaji ya Paris mwezi Novemba na ya hivi karibuni huko Brussels Ubelgiji. Papa Francis alikashifu mauaji yaliyotokea Ufaransa na Ubelgiji akisema kuwa hizo ni njama za watu wenye kiu cha kumwaga damu ya binadamu. Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alilaumu mtazamo wa watuhumiwa hao kuhusu maafa waliyosababisha. Aidha Baba Mtakatifu amewashauri watu wa dini tofauti duniani kuishi kwa amani. ''Haijalishi iwapo tunaimani tofauti la muhim...

ENGLISH SUMMARY OF POPE'S HOLY WEEK GENERAL AUDIENCE

Image
 ‘As we prepare to celebrate the Paschal Triduum in this Holy Year of Mercy, we are invited in a special way to contemplate the revelation of God’s infinite mercy in the events of Jesus’ passion, death and resurrection.’ Speaker:  Dear Brothers and Sisters:  As we prepare to celebrate the Paschal Triduum in this Holy Year of Mercy, we are invited in a special way to contemplate the revelation of God’s infinite mercy in the events of Jesus’ passion, death and resurrection.  Tomorrow, Holy Thursday, Jesus gives himself to us as food and, in the washing of feet, teaches us the need to serve others.  On Good Friday, in the mystery of Christ’s death on the cross, we contemplate that undying divine love which embraces all mankind and summons us in turn to love one another in the power of the Spirit.  Holy Saturday, the day of God’s silence, invites us not only to solidarity with all who are abandoned and alone, but also to trust in that faithful love whi...

LEO MAGAZETI YANA KIPI?

Image