Prof Makubi: Corona bado ipo wananchi msibweteke
MGanga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amewataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya ugonjwa wa covi 19 unaosababishwa na virusi vya corona. Prof. Makubi ameeleza hayo hivi karibuni alipokuwa anazungumza na Gazeti Kiongozi kuhusu kile kinachosadikiwa na jamii kuwa tayari kuna dawa ya corona. “Ninachiotaka kuwaambia wananchi ni kwamba, hakuna dawa ya corona. Mpaka sasa dawa haijapatikana nna ile tuliyoleta kutoka Madagascar bado inafanyiwa uchunguzi kujiridhisha. Wananchi hawa vijana na wale waishio vijijini wanapaswa waelewe kuwa, virusi vya corona havibagui umri wala mahali. Vijijini corona ipo tena ni rahisi kusambaa hasa kwenye minada na magulio. Hivyo waendelee kuchukua tahadhari kama zinavyoelekezwa na serikali pamoja na wataalamu wa afya ikiwemo WHO. Amewataka wenyeviti wa Mitaa, Vijiji, kata nk. kuweka mikakati ambayo itawasababisha wananchi waendelee na shughuli zao za kiuchumi. ...