Katibu Mkuu TEC: Wananchi msikebehi maelekezo ya serikali dhidi ya corona
JAMII imetakiwa kutokuzikebehi na kuzibeza juhudi zinazofanywa na serikali katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona, badala yake itekeleze kwa vitendo maagizo na miongozo inayotolewa. Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima katika mahojiano maalum na vyombo vya Habari nchini, yaliyofanyika katikati ya juma ofisini kwake Kurasini jijini Dar es Salaam. Amesema, Kanisa Katoliki nchini linaridhishwa na hatua zinazofanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya katika mapambazo dhidi ya ugonjwa huu ulionea sehemu mbalimbali duniani, hivyo akasisitiza kwamba hakuna sababu ya baadhi ya watu ama makundi ya kijamii kuzibeza na kuzikebehi juhudi hizo. Katika kusisitiza zaidi amesema “Tuiache Serikali ifanye kazi yake kwa kutumia wataalam wa afya iliyonao na kila mmoja kwa nafasi yake, atoe ushirikiano kama inavyotakiwa…hili siyo tatizo la kukebehi wala kufanyia mzah...