Maaskofu, mapadri, watakiwa kuhamasisha waamini kushiriki Kongamano la Ekaristi Takatifu
MAjimbo ya Kanda (metropolitani) ya Magharibi yaaswa kuhamasisha zaidi waamini wao kwa namna ya pekee kwenye maandalizi ya Kongamano la nne la Ekaristi Takatifu kitaifa litakofanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora. Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhashamu Paul Ruzoka hivi karibuni katika kikao cha saba cha maandalizi ya Kongamano hilo kilichohudhuriwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya. Akizungumza katika kikao hicho Askofu Ruzoka amewaomba wajumbe kutoka majimbo ya Tabora, Kahama, Kigoma na Mpanda kuwa mabalozi wa kuhamasisha waamini juu ya tukio hilo muhimu litakatolofanykika 1-5 July mwaka huu. Aidha amewakumbusha wajumbe kusali sala maalum katika majimbo yote ya Tanzania kuliombea Kongamano hilo. Vile vile ameagiza Kurugezi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Tanzania ihakikishe kwamba vyombo vya habari vya majimbo yote vinas...