Maaskofu wataka mapadri kutoa mahuribi hai si vijembe
Na Padri Anthony Chilumba RAis wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Mhashamu Gervas Nyaisonga amewataka Wahubiri wa Neno la Mungu kuzingatia kanuni bora za utoaji mahubiri yao kwenye maadhimisho mbalimbali ya Liturujia. Ameyasema hayo wakati anafungua Warsha ya Uboreshaji wa kutoa Homilia iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania iliyowakutanisha wajumbe wapatao 60 toka majimbo 26, wakiwemo Manaibu wa Maaskofu kutoka majimbo 15. Askofu Nyaisonga amewaambia washiriki hao kuwa, waamini wanaguswa sana na mahubiri yanayotolewa kanisani,hivyo ingawaje ni ya muda mfupi yanahitajika sana ili kuwatia moyo wakristo wanaoyasikiliza. Kwa mujibu wa Askofu Nyaisonga Ibada mbalimbali zinazoongozwa na mapadri zinapaswa kuwa hai na kwamba uhai huo unachangiwa na mahubiri ya adhimisho husika. “Mahubiri yenu yasidorore wala yasikinaishe wasikilizaji kwa sababu ya...