Wanaume Katoliki DSM waanzisha Bima ya Afya, Maisha
Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Jude Thadeus Ruwaichi akimkabidhi Mwenyekiti wa UWAKA Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Ndugu Amedeus Mosha kadi za Bima ya Afya mara baada ya kuzindua Mradi huo Dar es Salaam katika sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Msimamizi wa Wanaume Wakatoliki iliyofanyika katika kituo cha hija Pugu (Picha na Philipo Josephat) Na. Philipo Josephat-Dar es Salaam U moja wa Wanaume wakatoliki wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam umeanzisha Bima ya Afya na Bima ya Maisha. Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadei Ruwaichi amezindua kadi za Bima hizo hivi karibuni baada ya kuhitimisha Ibada ya Misa Takatifu siku ya wanaume katoliki (UWAKA) katika Sherehe ya Msimamizi wao Mtakatifu Yoseph iliyofanyika kwenye kituo cha hija Pugu jiji Dar es Salaam. Askofu Ruwaichi amewapongeza wanaume Katoliki Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam kwa ubunifu mkubwa wa...