UJUMBE WA BABA MTAKATIFU KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA WAGONJWA DUNIANI FEBRUARI 11, 2019
“MLIPOKEA BILA MALIPO, TOENI BILA MALIPO” (MT.10:8) Wapendwa Kaka na dada zangu, “Mlipokea bila malipo, toeni bila malipo”(Mt 10:8). Hayo ni maneno yaliyotamkwa na Yesu Kristu alipowatuma mitume wake kwenda kueneza Injili,ili ufalme wake uweze kuenea kupitia matendo ya ukarimu na upendo. Mlipokea bila malipo, toeni bila malipo (Mt 10:8). Katika kuadhimisha Siku ya Wagonjwa Duniani, itakayoadhimishwa rasmi tarehe 11-2-2019 huko Calcutta, India, Kanisa- kama Mama kwa watoto wake wote, na hasa walio wagonjwa, linatukumbusha kuwa ishara ya ukarimu na upendo kama wa yule Msamaria Mwema kama njia thabiti ya Uinjilishaji. Kuwajali na kuwatunza wajonjwa inahitaji utaalamu, upole, unyoofu na unyenyekevu unaotolewa bila kujibakiza, matunzo yanayomfanya yule anaye hudumiwa kuonja kupendwa. Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu.Mt. Paulo anauliza “ Ni kitu gani ulicho nacho ambacho hukupokea? (Kor. 4:7). Ni ukweli na dhahiri kabisa kwa sababu ulicho na ulichonacho ni zawadi, maish...