Padri awakumbusha waamini umuhimu wa kupokea Ekaristi

Waamini wenye sifa za kukomunika nchini wametakiwa kuacha tabia ya kukaa bila kushiriki kula mwili wa Kristo mara wanaposhiriki ibada mbalimbali..
 Akizungumza katika mahubiri kwenye ibada ya Misa takatifu Kigangoni Mbutu, Paroko wa parokia ya Kimbiji Padri Askecher Luciano amesikitishwa na idadi ndogo ya wakristo wanaojitokeza kushiriki kupokea Ekaristi Takatifu.
Amesema kupokea Ekaristi Takatifu ni kula mwili wa Yesu mwenyewe aliyewaamuru waamini kushiriki fumbo hili.
“Yesu mwenyewe baada ya kufa na kufufuka aliwatokea vijana wawili waliokuwa wanazungumza habari zake, kisha naye aliwafumba macho wasimjue na baadaye walimtambua katika kuumega mkate,” amesema padri Luciano.
Aidha amewaasa waamini wakristo kutokuogopa kuungama na kwamba amri ya Kanisa inayosema ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka haimfanyi Mkristo kuungama mwaka mzima mara moja bali kila itakapobainika kuwa kuna baya au dhambi imetendeka.
Wakati wa Kwaresima imeshuhudiwa mapadri kwenye baadhi ya Parokia wakipokea idadi ndogo ya waaamini waliokwenda kuungama, tofauti na idadi kamili ya wakristo sehemu husika.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU