Posts

Askofu Dallu akemea uchumba sugu

Image
Na Sr. Tuzo Nyoni OSB, Songea WAamini wameaswa kuachana na tabia ya kuishi uchumba sugu bila kufunga ndoa. Badala yake wafunge ndoa ili wapate kupokea sakramenti mbalimbali katika kanisa. Hayo yamesemwa hivi karibuni na Askofu Mkuu Damian Dallu wa jimbo Kuu Katoliki   Songea, wakati akihubiri katika Misa Takatifu ya jubilee ya miaka hamsini    ya Parokia ya Mtakatifu Martin wa Tur Mpandangindo iliyopo katika jimbo Kuu Katoliki Songea. Askofu Dallu amesema kuwa, suala la uchumba sugu limekuwa likijitokeza katika parokia nyingi jimboni Songea na kuhimiza kuwa, waamini hawana budi kushika amri za Mungu na Kanisa kikamilifu. Ameongeza kuwa, suala la kutoa zaka kwa waamini ni la msingi na kwamba waamini waachane na tabia ya kutoa zaka kwa Kanisa wakati wanapokuwa na majukumu ya kusimamia na kupokea sakramenti tu. Akizungumzia sherehe ya Jubilei ya miaka 50 ya parokia hiyo ya Mpandangindo Askofu Dallu amesema , anatoa shukrani kwa uwepo wa wamisionari Wabene...

Jubilei miaka 75 Masista wa Upendo

Image
‘Mkiushinda ubinafsi mtafanikiwa’ Na Pascal Mwanache, Mbingu MASISTA wa Shirika la Upendo wa Mt. Fransisko Mahenge wameaswa kufanya kazi kwa kushirikiana huku wakiweka kando ubinafsi ili kazi zao ziendelee kumtukuza Mungu. Hayo yameelezwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Tundu-Masasi Mhashamu Filbert Mhasi katika Misa Takatifu ya kuwakumbuka marehemu waanzilishi wa shirika hilo la masista pamoja na masista waliofariki, ikiwa ni sehemu ya sherehe ya jubilei ya miaka 75 ya shirika la masista wa upendo wa Mt. Fransisko Mahenge. Akitoa homilia katika misa hiyo Askofu Mhasi amewaasa masista hao kutotafuta mtetezi mwingine zaidi ya Mungu pale wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali katika utume wao, bali wadumu katika uthabiti wa imani yao na Mungu atawatetea. “Inatupasa kumshukuru Mungu kwa imani tuliyojaliwa kupitia Kristo. Waanzilishi wa shirika hili walipigana vita vizuri na waliamini kuwa kuna maisha baada ya kifo. Ndiyo maana wakawa imara katika imani yao. Hawakuwa wabinaf...

Msitumie vibaya utajiri wenu -Askofu Kinyaiya asema

Image
Na Ndahani Lugunya na Rodrick Minja, Dodoma Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya, amekemea tabia ya baadhi ya wakristo waliopewa utajiri na Mwenyezi Mungu kuutumia vibaya utajiri huo hususani kwa kuwanyanyasa wanyonge, yatima, masikini na wasiojiweza. Ameyasema hayo wakati akitoa homilia yake kwenye adhimisho la sadaka ya Misa Takatifu, katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Damu Azizi ya Yesu-Kisasa Jimboni Dodoma, Misa iliyokwenda sambamba na utoaji wa sakramenti Takatifu ya kipaimara kwa vijana 76 wa Parokia hiyo. Katika homilia yake Askofu Kinyaiya amesema kuna baadhi ya wakristo wamejaliwa kupata utajiri kwa halali kabisa, lakini kosa linakuja pale mtu anapoutumia utajiri huo kwa ubadhilifu na kuzitumia katika matumizi yake ya kila siku pasi na mpangilio mzuri. “Mmejaliwa utajiri na Mwenyezi Mungu hivyo utumieni kwa kutenda mema na sio kunyanyasa wengine ambao hawakujaliwa utajiri huo kwani hata ipo siku mwenyezi ...