Posts

Jamii yatakiwa kuthamini wazee

Image
Jimmy Mahundi, Mtwara Jamii imetakiwa kuacha tabia ya kuwatelekeza wazee na kuwaacha waishi katika mazingira magumu. Kauli hiyo imetolewa na wazee walioshiriki kongamano la wazee katika kuadhimisha siku ya wazee duniani ambapo kitaifa imefanyika mkoani Mtwara na kuhudhuliwa na wawakilishi wa wazee kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Wazee hao wamedai kuwa kwa sasa wengi wao wanaishi maisha magumu sana kutokana na vijana wao waliowasomesha kwa shida na taabu leo wanawaona mizigo na wanashindwa kuwasaidia. “Baadhi ya watoto wetu wanatuona kama mizigo maana hatuna nguvu tunawategemea kwa kila kitu. Pia wanasahau kutimiza wajibu wao wa kulea   wazazi wao kama sisi tulivyotimiza wajibu wetu kuwalea na kuwasomesha. Hivyo wanaposahau kuwa nasi pia tuliwalea na kuwapa elimu, wanajiona kuwa   mafanikio wanayopata ni kutokana na juhudi zao tu. Inasikitisha kuona wazee   wanaishi maisha magumu sana kwa kuwa watoto wao wanawaona kuwa ni mizigo isiyobebeka”amesema Mzee...

Metropolitani ya Tabora yazindua Kongamano la Ekaristi Takatifu

Image
Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora akiwa ndani ya kanisa Kuu la Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu Yesu Tabora. Na. Thomas Mambo -Tabora. Majimbo yanayounda Kanda ya Magharibi (Metropolitani ya Tabora) hivi karibuni imefanya uzinduzi wa Kongamano la Ekaristi Takatikafu katika Makao Makuu ya Kandahiyo   katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora ikiongozwa na kauli mbiu “Ekaristi Takatifu , Chemchemi ya Uzima Wetu.” Misa hiyo ya uzinduzi iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhashamu   Paul Ruzoka imefanyika hivi karibuni   katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu jimboni Tabora. Askofu Ruzoka amesisitiza umuhimu wa kutumia mali na majaliwa ambayo Mungu anampatia kila mmoja   ili yamsaidie katika maisha yake ya hapa duniani na baadaye katika uzima wa milele. Aidha amesema kuwa katika ulimwengu wa sasa mwanadamu anaweza kutekwa nyara na mali za dunia hii akasahau kuona na kujali shida ya jirani yake. “...