Askofu Ruzoka awafunda waseminari waliohitimu Falsafa Kipalapala
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mashamu Paul Ruzoka amwewaasa Mafrateri wa seminari Kuu Ya Mtakatifu Paulo Mtume Kipalapala kuwa waaminifu kwa Neno la Kristo na kumfuata Kristo kwa kuishi maisha ya ufukara na kukaa mbali na mali za dunia. Rai hiyo ameitoa hivi karibuni katika Kanisa la seminari hiyo alipokuwa akitoa mahubiri yake yaliyolenga kumshukuru Mungu kwa neema nyingi alizowajalia mafrateri wa mwaka wa nne waliohitimu malezi yao seminarini hapo. Akizungumza wakati wa Misa Takatifu Askofu Mkuu Ruzoka amewahimiza mafrateri hao wanaoenda kufanya utume wao katika sehemu mbalimbali za majimbo ya Tanzania kuishi yale walioyapata wakati wa malezi yao . “ Nendeni mkatoe harufu nzuri ili kwa wale mtakaowahudumia wamuone Kristo kupitia nyie”, Askofu Ruzoka amesema. Aidha katika mahubiri yake Askofu Ruzoka amewaomba mafrateri wahitimu kujua sasa wameongezeka kimo na ufahamu hivyo hawanabudi kutumia elimu na maarifa waliyoyapata kwa faida ya Kanisa na wanapaswa kuhakikish...