Posts

Askofu Lebulu aadhimisha Jubilei ya Dhahabu ya Upadri

Image
  Na Sarah Pelaji, Same-Kisangara Juu A skofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha Mhashamu Josaphat Lebulu ameadhimisha Jubilei ya dhahabu ya   Upadri   yaani miaka 50 tangu alipopata Daraja Takatifu la Upadri. Jubilei hiyo imeadhimishwa Desemba 11 mwaka huu katika Parokia ya Kisangara Juu Jimbo Katoliki Same ambapo parokia hiyo pia imeadhimisha miaka 50 tangu ilipoanzishwa na katika parokia hiyo ndipo Askofu Mkuu Mstaafu Lebulu alipewa Daraja Takatifu la Upadri na   Askofu Joseph Kilasara Desemba 11 mwaka 1968. Katika maadhimisho hayo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Gervas Nyaisonga amesema kuwa, kwa niaba ya Maaskofu wakatoliki Tanzania, anampongeza Askofu Lebulu kwa kufanya kazi ya utume uliotukuka huku akimsihi aendelee kulisaidia Kanisa akitumia hekima na vipawa alivyojaliwa. “Ni wazi Askofu Lebulu amestaafu na anaadhimisha jubilei hii ya dhahabu lakini bado ana nguvu na anahitajika katika Kanisa. Sisi tunamuombea M...

Changamoto zinatusaidia kujua umuhimu wetu nchini- Rais TEC

Image
Na Pascal Mwanache, Mwanza A SKOFU wa Jimbo Katoliki Mpanda ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga amewataka wahitimu waliohitimu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) kukabiliana na changamoto mbalimbali watakazokutana nazo ambazo zitakuwa kinyume na matarajio yao, na kwamba changamoto zinasaidia kujua umuhimu wa mtu au taasisi. Amesema hayo katika mahafali ya 20 ya SAUT yaliyofanyika katika viwanja vya Raila Odinga chuoni hapo Desemba 7, 2018, na kusema kuwa hata SAUT inakutana na changamoto ambazo ni kinyume na matarajio ya uanzishwaji wa chuo hicho miaka 20 iliyopita. “Changamoto zinatusaidia kujua tuna nguvu kiasi gani, na kujiwekea viwango. Matarajio yenu yanaweza yasiwe sawa na mlivyotazamia. Ni sawa na Baraza la Maaskofu   lilipoanzisha vyuo hivi. Matarajio siyo kama tunavyoona. Chuo mama SAUT kinahitimu sasa mahafali ya 20. Kilikuwa na matarajio makubwa. Lakini mnajua kwamba tunapita katika ...

Polisi wajipanga kudhibiti uhalifu msimu wa Krismas

Image
Na Erick Paschal,Dar es Salaam. K uelekea sikukuu za mwisho wa mwaka Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limeimarisha ulinzi katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam,hususani katika taasisi mbalimbali za fedha (benki),maduka ya kubadilishia Fedha za kigeni na sehemu zenye mkusanyiko wa maduka mengi . Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka kumekuwa na baadhi ya watu ambao hujitafutia kipato kisicho cha halali kwa kufanya vitendo vya kiuhalifu,hivyo kutokana na hali hiyo jeshi la Polisi Kanda maalumu limejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba hakuna tukio lolote la uhalifu litakalojitokeza. Kamanda Mambosasa alizidi kuongezea kwa kuwataka wanachi wasiwe na hofu pindi watakapoona   idadi kubwa ya Askari wakifanya doria katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam   na badala yake watoe ushirikiano kwa kutoa ta...