Heri tufe kwa njaa kuliko misaada yenye shinikizo la ushoga-Kard. Pengo
Na Philipo Josephat - Dsm A SKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amepongeza na kufurahia msimamo wa serikali dhidi ya kauli ya baadhi ya mataifa ya Magharibi kutishia kusitisha misaada kwa Tanzania kwa kuwa nchi inapinga ushoga. Ametoa msimamo huo hivi karibuni katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya Mavuno iliyofanyika kijimbo katika Viwanja vya Msimbazi Centre, vilivyopo Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam. Kardinali Pengo amesema kuwa yapo baaadhi ya mataifa yanayotishia kukata misaada kwa nchi zinazopinga ushoga na mahusiano ya watu wa jinsia moja hivyo Kardinali Pengo amesisitiza kuwa, ni heri kufa kwa njaa kuliko kupokea misaada yenye shinikizo la kufanya mambo machafu yaliyo kinyume na Mungu. Kiongozi huyo wa kiroho amesema kuwa, uchafu wa mahusiano ya watu wa jinsia moja ndio uliosababisha Sodoma na Gomora kuangamizwa na kwamba, mambo hayo ni kinyume na mpango wa Mungu katika uumbaji, hivyo hayawezi kukubalilik...