Balozi wa Baba Mtakatifu afanya ziara ya kichungaji Jimboni Musoma
Na Veronica Modest- Musoma B alozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski amefanya ziara ya kichungaji kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake,katika Jimbo Katoliki Musoma kuan zia Oktoba 02 hadi 09 mwaka huu. Katika ziara hiyo Balozi huyo ametembelea maeneo mbalimbali ambapo Oktoba 02 alikuwa katika Parokia ya Kiabakari na aliongoza Ibada ya uzinduzi wa kituo cha Hija ya Huruma ya Mungu Kiabakari na kukipandisha kutoka hadhi ya Kijimbo hadi hadhi ya Kitaifa pamoja na kubariki Kikanisa (chapel) cha Bikra Maria. Ametembelea kliniki ya meno na macho katika kituo cha afya cha Blessed Pier Giorgio Frassati Kiabakari na kubariki wagonjwa. Akiwa Parokiani hapo alikutakutana pia na mapadri ,watawa na waamini wa udekano wa Butiama. Oktoba 03 Balozi huyo akiwa katika Kanisa Kuu la Musoma alishiriki kusali Rozari Takatifu na waamini wa parokia hiyo na aliongoza ibada ya Baraka Kuu na baadae alikutana na ...