Na Na Pascal Mwanache, Dar es salaam L ikiwa linaadhimisha Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara, Kanisa Katoliki nchini limeendelea kuwa kielelezo katika utoaji wa huduma za elimu, afya na za kijamii bila upendeleo hasa kwa watanzania wanaoishi maeneo ya vijijini. Akifungua Mkutano Mkuu wa Idara ya Afya ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda Mhashamu Renatus Nkwande amesema kuwa Kanisa litaendelea kutoa huduma za afya na elimu nchini kwa kufuata yale yaliyofanywa na Kristo, ambaye alitibu na kufundisha. “Endeleeni kushiriki kikamilifu, shirikishaneni mang’amuzi yenu katika utoaji huduma ili kuwafanya wale tunaowahudumia waone kuwa ufalme wa Mungu umetamalaki” ameeleza Askofu Nkwande ambaye pia ni Mwenyekiti wa Idara ya Afya TEC. Aidha Askofu Nkwande ametoa rai kwa wajumbe wa mkutano huo kujikita katika kufanya utafiti, uvumbuzi na mafunzo badala ya kujikita katika kutibu peke yake. Kwa upande wake Katibu Mkuu ...