Posts

Maaskofu wa Chile wakutana na Papa mkutano wa dharura

Image
Roma M AASKOFU wa Chile wapo Roma wiki hii kwa ajili ya mkutano wa dharura na Papa Fransisko, ambaye anataka kukabiliana na mgogoro wa unyanyasaji wa kijinsia uliojificha katika Kanisa nchini mwao. Maaskofu   thelathini na moja wa Chile watashiriki, pamoja na wachache   waliostaafu. Mkutano huo utaanza Mei 15-17 ambapo Kardinali Cardinal Francisco Javier Errázuriz wa Chile anahusika zaidi na   mzozo huo kwani anashutumiwa na waathirika wa unyanyasaji na Mahakama ya Jinai ya Vatikani kufunika kesi ya Padri Fernando Karadima, ambaye alikuwa kuhani maarufu nchini Chile, baada ya kupata hatia ya unyanyasaji wa kijinsia miaka kadhaa iliyopita. Taarifa kutoka Vatikani zimeeleza kuwa, mkutano utafanyika kwa siri, na kwamba Baba Mtakatifu angewasilisha maaskofu wa Chile kwa hitimisho lake kwa misingi ya hati ya 2300 ya uchunguzi wake maalum. Maaskofu wa Chile wanasema kuwa, makosa yalifanyika wakati wa kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia wa...

Kila muumini awe mmisionari-Padri asisitiza

Image
Na Ivetha Kimburu ± Dar es salaam W ANAUTUME wa Fatima hapa nchini, wameelezwa kuwa kupitia ujumbe wa Fatima uliotolewa na Bikira Maria kule Ureno alipowatokea Watoto wa Tatu, Russia, Fransisko na Yasinta wanaalikwa kuwa wamisionari wa kweli na hasa kuwaombea wale wote wasiomwamini Kristo, ili wapate kumwamini na kufuata matendo yake. Wito huo kwa Wanautum hao wa Fatima umetolewa na Padri Evans Msechu, wakati akiadhimisha sadaka ya Misa Takatifu kwenye adhimisho la siku ya Bikira Maria Mama yetu wa Fatima iliyofanyika katika Parokia ya Msimbazi Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam. Padri Msechu ambaye ni katibu wa Ndugu wadogo wa Fransiskani amesema kuwa, Mama Bikira Maria ni mmisionari wa kwanza, na kwa kuwa Wanautume wa Fatima wanamwakilisha yeye hawana budi kuwa wamisionari katika maisha yao yote na mahali popote pale wanapokuwa. Aidha ameongeza kuwa wanautume wa Fatima wanapaswa kutambua kuwa wao ni mabalozi, na kazi kubwa ya Balozi ni kuwakilisha jam...

‘Wakatoliki ishini ukatoliki wenu’

Image
Na Ivetha Kimburu, Iringa W AAMINI wa Kanisa Katoliki wametakiwa kuishi maisha yaliyo mema katika Familia, Jumuiya , mitaa yao pamoja na jirani zao, ili Mwenyezi Mungu aweze kuidhihirika ndani mwao kila siku za maisha yao. Hayo yameelezwa na   Makamu wa Askofu wa jimbo Katoliki la Iringa ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Ifunda Padri, Vicent   Mwagala wakati wa mahubiri yake kwa Waamini wa Parokia hiyo wakati akiadhimisha Sadaka ya Misa Takatifu ya kupaa Bwana. Padri Mgwagala amesema kuwa, Mungu kamwe hawezi kujitenga nao na daima yuko kati yao kupitia Roho Mtakatifu ,ambaye anawaangazia ili Kristo aliyepaa Mbinguni aendelee kuishi ndani yao, kwani katika Kristo Waamini Wote wanatumaini kuufikia ufamle wa mbingu. Ameongeza Kuwa zawadi ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Mungu inawasaidia Waamini kutambua kuwa, wao wameunganika na Kristo aliyekichwa cha Kanisa, na kupitia kwake ndipo nao wataweza kufika mbinguni kwa Baba, lakini ili waweze kufika huko ni l...