Posts

Waliosoma Chanjale seminari wamuunga mkono Askofu Kimaryo kuendeleza jimbo

Image
Na Philipo Josephat Same Kilimanjaro W anamalezi wote waliosoma katika seminari ya Chanjale tokea ilipoanzishwa wameungana na Askofu wa Jimbo Katoliki Same Mkoani Kilimanjaro Mhasham Rogathy Kimario kuendeleza utume katika jimbo hilo. Awali walianza kujumuika katika hija ya kusali njia ya msalaba siku ya Ijumaa Kuu kwa kupandisha mlima kuanzia Njoro hadi Chuo cha Malezi Dido ambapo wanafunzi wanapata elimu ya awali ya sekondari (pre-form one) kabla ya kuingia kidato cha Kwanza huko Chanjale Seminari wilaya ya Mwanga Kilimanjaro.   Kwenye hija wanamalezi hao waliosoma katika Seminari hiyo miaka ya 1983 hadi 2015 wameahidi kumuunga mkono Askofu Kimaryo   katika kulipeleka mbele jimbo Katoliki Same. Wanamalezi hao wakiongozwa na Ndg Karol Kadeghe na Goodluck Kavugha   walimkabidhi Askofu Kimaryo Television moja kama zawadi kwa watoto wanaosoma katika Chuo cha Malezi Dido, vazi la Askofu la kuendeshea ibada na kumuonesha ujenzi wa vyoo na mabafu ...

Papa akutana na Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria

Image
B araza la Maaskofu Katoliki Nigeria, kuanzia Aprili 24-30, 2018 linafanya hija ya kitume mjini Vatikani kwa kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Fransisko pamoja na waandamizi wake. Hii ni hija ambayo kadiri ya sheria kanuni za Kanisa hufanyika walau kila baada ya miaka mitano! Kanisa Katoliki nchini Nigeria linaundwa na Majimbo makuu 9 na chini yake kuna majimbo 45. Ni Kanisa ambalo bado ni changa, lakini linakabiliwa na changamoto, matatizo na fursa katika maisha na utume wake wa kumtangaza na kumshuhudia Kristo Yesu aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu!   Uongozi mbaya, rushwa na ufisadi wa mali ya umma; ukabila, udini na misimamo mikali ya kiimani ni kati ya mambo yanayoendelea kusababisha vita, kinzani na mipasuko ya kijamii na kidini sehemu mbali mbali za Bara la Afrika, lakini Nigeria kwa namna ya pekee kabisa! Wanaigeria ni watu wa dini na kwamba, imani ni sehemu muhimu sana ya utambulisho na maisha yao. Sehemu kubwa ya wananchi wa Nigeria ni waamini wa din...

PICHA YA SIKU

Image

Baadhi ya matukio yaliyojiri katika uzinduzi wa ujenzi wa Hostel za Jimbo Katoliki Mbeya, kama ulivyozinduliwa na Askofu Evarist Chengula wa jimbo hilo.

Image

MASOMO YA MISA, APRILI 25, 2018

Image
MASOMO YA MISA, APRILI 25, 2018 JUMA LA 4 LA PASAKA, JUMATANO SIKUKUU YA MTAKATIFU MARKO, MWINJILI SOMO 1 1 Pet 5: 5-14 Ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika ¡mani, mkijua ya kuwa mateso yale yaie yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika «risto, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu. Uweza una yeye hata milele na milele. Amina. Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikia kwa maneno machache...

MTAKATIFU WA SIKU

Image
MTAKATIFU MARKO MWINJILI NA MTAKATIFU EUFRASIA PALLETIER, MTAWA Leo Mama Kanisa anamkumbuka na Kumheshimu Mtakatifu Marko Mwinijili wa (Karne ya Kwanza) na Mtakatifu EUFRASIA PELLETIER Mtawa na Mwanzilishi wa Shirika. Mtakatifu Marko Habari za kale zinasimulia kuwa Mtakatifu Marko alikuwa Binadamu ya Mt. Barnaba na mmoja wa Wanafunzi waliomfuata Yesu Kristo. Lakini Mtakatifu Epifani anatuhadithia kuwa Mtakatifu Marko na wenzake walikataa kusadiki kwanza walipo ambiwa na Bwana wetu maneno haya . “  Msipokula mwili wa mwana na mtu, msipokunywa damu yake hamtakuwa na uzima ndani yanu”. Mtakatifu Petro alimuongoza Marko kisha kufufuka kwake Bwana wetu, akamfanya kama mwandishi wake. injili iliyoandikwa na Marko ni kama jumla ya mafundisho yalimofundishwa na wakuu wa mitume ,hata walimu wakanisa husema ni Injili ya Mtakatifu PETRO. Marko ametusimulia habari nyingine zisizo andikwa katika Injili nyingine, kama vile sifa ya yule mjane masikini aliyetoa sadaka yake hekaluni. Ni ...