Posts

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMANNE YA FEBRUARY 20

Image

KIONGOZI MKRISTO ASIYEWAJIBIKA AJITATHMINI NDANI YA KWARESIMA

Image
Mwanasheria na Mhadhiri wa kimataifa kuhusu Afrika P.L.O Lumumba aliwahi kusema kuwa moja ya matatizo makubwa Afrika ni kwamba Viongozi wengi wa Afrika hawana sifa ya kuwa Viongozi. Kwa miaka miwili sasa anaisifia Tanzania kuwa ni kinara cha kuigwa Afrika. Muda huu wa Kwaresima wale wote wenye nyadhifa za uongozi wa dini na serikalini wajihoji kuhusu majukumu waliyopokea. Musa alilelewa kwenye ikulu ya Farao, mfalme wa Misri kwa muda wa miaka 40. (Mdo 7: 20 -23) Kwa miaka 40 alifanya kazi ya kuchunga kondoo wa Baba Mkwe wake Yethro huko Midiani (Mdo 7:30). Akiwa na umri wa karibu wa miaka 80 Mungu alimpa kazi mpya ya kuongoza watu na kuwatoa Utumwani (Mdo 7:30 - 34). Musa alimwambia Mungu ‘Kwanini umenitwisha mzigo wa watu hawa juu yangu’ (Hesabu 11:11-12). Kiongozi anabeba Taifa lote kichwani mwake, Musa alihoji kila mara ‘nipate wapi nyama ya kuwapa watu wote hawa’ (Hes 11:13). Sehemu nyingine alihoji ‘nipate wapi maji ya kuwapa watu wote hawa wanywe’ Musa alikiri mbele ya M...

Baba Mtakatifu Fransisko akiwasili katika kituo cha kiroho huko Ariccia karibu na Roma kwa ajili ya kuanza mafungo ya kiroho katika kipindi hiki cha kwaresima

Image

KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA ASK. MKUDE ATAHADHARISHA

Image
‘Haki itendeke kwa wote’ Na Pascal Mwanache, Morogoro NCHI inapojiandaa kutekeleza haki ya msingi ya kidemokrasia ya raia wote kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji hapo 2019 wito umetolewa kwa vyombo husika kuwa walinzi wa watanzania wote kwa haki bila kuminya haki za watu wengine. Wito huo umetolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki Morogoro Mhashamu Telesphor Mkude katika Misa Takatifu ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mt. Patriki Morogoro. Askofu Mkude amesema kuwa kila mmoja anapaswa kujitathmini iwapo amekuwa mlinzi wa mwingine au amewatendea mema wale tu waliokuwa upande wake. “Tunapojiandaa na uchaguzi mdogo katika serikali za mitaa tujiulize, mtazamo wetu juu ya jirani upoje? Tumekuwa walinzi kweli. Tumekuwa walinzi wa watanzania wote? au tunakwenda na mawazo gani, kwamba ndugu kwangu mimi ni yule ninayetoka naye mtaa mmoja, au familia moja tu? Mwingine siyo ndugu yangu?   Kama mkiwapenda wale wanaowapenda t...