Posts

‘Kanisa siyo mshindani, ni mtumishi’ Ask. Ngalalekumtwa

RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema kuwa Kanisa halina wazo lolote la ushindani katika utoaji wa huduma zake, bali linafanya hayo yote kwa kuwa huo ni utume na wito wake. Ameeleza hayo katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 ya Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii nchini (CSSC), yaliyofanyika jijini Dar es salaam, na kubainisha kuwa Kanisa linatumia rasilimali zake kwa ajili ya ustawi wa taifa na watu wake. “Kanisa siyo mfanya biashara, na siyo mshindani ila ni mtumishi. Kanisa linaendelea kutoa huduma bora ikiwemo elimu bora na siyo bora elimu, afya na kuwatunza wenye dhiki. Hatuna nia ya kuingia ushindani, tunatumia rasilimali zetu kwa ajili ya taifa letu ili liwe lenye heshima, utu na ustawi” ameeleza Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa CSSC. Kauli hiyo imeungwa mkono na Rais wa CSSC Askofu Alex Malasusa aliyeweka wazi kwamba makanisa hayatoi huduma za afya na elimu kwa ajili ya kupata faida kiuchumi. Amese...

SOMA GAZETI LA KIONGOZI LEO IJUMAA FEB 24

Image

‘Hakuna maendeleo bila Kanisa’ Mwinyi asema

Image
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa Kanisa ni chombo muhimu katika maendeleo ya jamii ya Tanzania, hasa kwa kuchangia katika kuweka mazingira chanya ya upatikanaji wa elimu na afya. Alhaji Mwinyi ameeleza hayo katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 ya Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii nchini (CSSC), yaliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni, ambapo amesema kuwa Kanisa daima liko mstari wambele katika katika kutoa huduma bora za elimu na afya nchini. “Mara zote huwa nawaambia jamaa zangu kule Temeke, nendeni katika hospitali za Kanisa. Wale wenzetu wanafanya ile kazi kama sehemu ya ibada yao. Nawaambia wazi wakienda huko watapata dawa na upendo” amesema Mwinyi. Ameongeza kuwa kutokana na ushirikiano huo baina ya makanisa nchini katika utoaji wa huduma, watanzania wengi wamepata huduma bora, na kuwaomba maaskofu waendelee kuithamini CSSC ili iendelee kustawi. Ameweka wazi kuwa jamii ya watanzania i...

Wanachuo msitumie dawa za kulevya-Ask. Mkude

Image
ASKOFU wa Jimbo Katoliki Morogoro Mhashamu Telesphor Mkude ametoa wito kwa vijana hususani waliopo vyuoni kutojihusisha na dawa za kulevya, kwani kufanya hivyo ni kusitisha ndoto na mafanikio waliyojiwekea maishani. Askofu Mkude ametoa wito huo alipokuwa akihubiri katika ibada ya Misa Takatifu iliyoambatana na uzinduzi na kubariki eneo la kufanyia ibada kwa wanafunzi   wa Chuo Kikuu cha kilimo Sokoine (SUA) Jumuiya ya Mtakatifu Don Bosco New Hostel iliyopo nje kidogo ya Chuo hicho katika   Parokia ya Maria Konsolata SUA. Katika mahubiri yake Askofu Mkude amekazia umuhimu wa wanachuo kuzitafakari kwa kina athari zitokanazo na dawa za kulevya kwa afya zao, hivyo watambue kuwa Mwenyezi Mungu amewaumba wakiwa wema ili kumtumikia siku zote za maisha yao. “Mwenyezi Mungu amewaumba vizuri ili mumtumikie yeye siku zote za maisha yenu ya hapa duniani hivyo ili kuliepuka hili janga la dawa za kulevya mnatakiwa mtafakari kwa kina athari zitokanazo na matumizi na uuzaji wake,” a...

‘Makanisa yataiwezesha Tanzania ya viwanda’ Dkt. Kigwangala

Image
KATIKA kuelekea uchumi wa viwanda nchini makanisa yametajwa kuwa mdau muhimu katika kufanikisha adhma hiyo, kwa jinsi yalivyoweka kipaumbele kwa utoaji huduma katika sekta za afya, elimu, sayansi na teknolojia. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 ya Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii nchini (CSSC), yaliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni na kuhudhuriwa na mamia ya wajumbe. Dkt. Kigwangala ameeleza kuwa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii imekua mdau muhimu katika kuratibu na kusimamia huduma za jamii hapa nchini, hususani huduma za elimu na afya, na hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini. “Kama mnavyofahamu, nchi yetu iko kwenye mpango wa kuelekea kwenye uchumi wa viwanda, lengo hili litafikiwa tu iwapo nchi yetu itakuwa na watu wenye afya bora na elimu ya kutosha ambao wataweza kushiriki kikamilifu na kutoa mchango wao katika kuf...

UZINDUZI JUBILEI YA MIAKA 100 YA UPADRI TANZANIA BARA, JIMBO KATOLIKI SAME

Image

MATUKIO MBALIMBALI JIMBO KATOLIKI SAME LIKIFUNGUA JUBILEI YA MIAKA 100 YA UPADRI TANZANIA BARA

Image