Posts
Showing posts from May, 2017
Kanisa Barani Afrika: Chombo cha haki, amani na upatanisho!
- Get link
- X
- Other Apps
Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Kupaa Bwana, Mbinguni, tarehe 25 Mei 2017, alikutana na kuzungumza na wakleri pamoja na watawa wa Jimbo Katoliki la Bata, huko Equatorial Guinea kwa kukazia utambulisho wao kama Kanisa familia ya Mungu inayowajibika, dhana iliyotiliwa mkazo sana katika maadhimisho ya Sinodi ya kwanza ya Maaskofu kwa ajili ya Kanisa la Afrika. Huu ni mwaliko wa kuendelea pia kushikamana na Kanisa la kiulimwengu katika mchakato mzima wa uinjilishaji, lakini kwa namna ya pekee na Askofu wao Juan Matogo Oyama. Kardinali Filoni anawapongeza wakleri na watawa kuwa mchakato mzima wa uinjilishaji unaofumbatwa katika ushuhuda wa huduma makini katika sekta ya elimu, afya, ustawi na maendeleo endelevu ya watu wa Mungu nchini Equatorial Guinea: dhamana, utume na asili ya Kanisa ambalo linatumwa na Kristo Yesu ili kuinjilisha. Uinjilishaji ni sehemu ya vinasaba vya maisha, utume na changamoto ...
WAWATA NA CARITAS WAWAPA MBINU WANAWAKE MBEYA
- Get link
- X
- Other Apps
IMEELEZWA kuwa wanawake ni nguzo ya familia,jamii na Taifa lolote duniani ,hivyo hawapaswi kujiona wanyonge na badala yake wajitume katika shughuli mbalimbali za kujipatia kipato bila kujibakisha ili waweze kuzilea vyema familia katika maadili mema na hata kufikia hatua ya kulitegemeza Kanisa. Hayo yamesemwa na Mratibu wa Jinsia,,Vijana na Watoto, Idara ya Caritas na Maendeleo,Jimbo Katoliki la Mbeya,Praxeda Manyuka katika ziara yao ya kuwatembelea Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu, Parokia ya Ilambo kujionea shughuli za maendeleo wanazozifanya ili kujiingizia kipato. Praxeda amesema kuwa wanawake kama walezi wa familia wanapaswa kujituma katika shughuli mbalimbali za kujitafutia kipato ili waweze kuilea vema familia,kaya na kwamba wanao uwezo mkubwa wa kulitegemeza kanisa. "Akina mama ndiyo nguzo ya familia,mnapaswa kujituma katika shughuli mbalimbali za maendeleo...tunaa...