J E, unazungumzaje kuhusu “chumaulete” ambapo inasemekana pesa za mtu mmoja zinaweza kwenda kwa mwingine kwa kufanya ushirikina? Jibu: Habari za “chumaulete” ni uongo wa kifukara. Ni uongo ambao kudhihirika kwake lazima ufikiri wa kinyume. Waafrika, katika dhiki zetu na ufukara wetu huwa na hadithi za kupata mali au pesa “kwa che”. Ndiyo kisa, kati yetu hustawi habari za kupata mali kwa uchawi au ushirikina, au kwa kutumia mapepo (yaani mashetani), au kwa kutumia majini, au kwa kupitia Frimasoni na kadhalika. Kila mara tuna maelezo ya ajabu kwa wanaokuwa matajiri kati yetu, yaani usiwe na nyumba au gari kuwazidi walio wengi mhali ulipo. Wengine tutasema ni wachawi. Wengine tutasema wanatumia mapepo au “majini” kama Waislamu waaminivyo. Wengine tutasema wanapata kwa kuwa ni wanachama wa Frimasoni na kadhalika. Kifupi, hatukosi maelezo sisi! Kumbe, kwa sababu ya dhiki zetu, Waafrika huwa tunaaminishana kwamba kuna njia za mikato za kupatia pesa au utajiri. Hiyo ndiyo imani in...