Posts

Showing posts from February, 2019

Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Filbert Mhasi

Image
Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi Mhashamu Filbert Mhasi akionyesha hati ya kuteuliwa kwake kuwa askofu wa jimbo hilo iliyotoka kwa Baba Mtakatifu Fransisko (Picha na Pascal Mwanache) Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi Mhashamu Filbert Mhasi akiwabariki waamini waliompokea katika Parokia ya Chikukwe, ambayo ni parokia ya kwanza ya Jimbo hilo iliyopo mpakani na Jimbo Katoliki Mtwara (Picha na Sarah Pelaji) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambaye ndiye aliyekuwa Askofu kiongozi mweka wakfu akimkabidhi Askofu Filbert Mhasi kitabu cha Injili katika Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mhasi (Picha na Pascal Mwanache) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akimvalisha pileolus (zucchetto) na mitra Askofu Filbert Mhasi (Picha na Pascal Mwanache) Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi Mhashamu Filbert Mhasi akiwa ameketi katika kit...

Askofu Mhasi asimikwa Tunduru Masasi

Image
Na Pascal Mwanache, Tunduru A SKOFU Filbert Mhasi amewekwa wakfu na kusimikwa kuwa wa Askofu wa nne wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi, katika adhimisho la MisaTakatifu lililofanyika katika Kanisa Kuu la Mtalatifu Fransisko Xavery na kushuhudiwa na mamia ya waamini. Akimkaribisha Askofu Mhasi katika urika wa maaskofu, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga amesema kuwa Kanisa jimboni humo na Taifa kwa ujumla halina budi kuishi katika misingi ya kufanya kazi pamoja kama familia moja yenye mshikamano na dira ya kufikia malengo yaliyokusudiwa. Aidha Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye pia ni Askofu Mkuu Mteule wa Jimbo Kuu teule la Mbeya ametoa rai kwa waamini wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi kushikamana na mchungaji wao mkuu na kudhihirisha tunu za familia yenye kushirikiana kwa ajili ya ustawi wao. “Ninatoa rai kwenu kuishi kwa mshikamo,mapendo na umoja ndani ya jimbo lenu. Mshikamane na askofu wenu mpya. Mdhihirishe maisha ya familia inayo...

Sera za nchi zisipingane na mpango wa Mungu-Ask. Dallu

Image
Na Pascal Mwanache, Tunduru W ATUNGA sera mbalimbali za nchi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa upendo na kwa kuwahusisha wadau wa sekta husika ili sera hizo sizipingane na mpango wa Mungu kwa watu wake. Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea Mhashamu Damian Dallu wakati akitoa homilia yake katika Ibada ya masifu ya jioni yaliyotangulia kusimikwa na kuwekwa wakfu Askofu Filbert Mhasi wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi. Askofu Dallu amesema kuwa Kanisa linaendelea kusali na kushukuru kwa hatua zile zinazochukuliwa na kuona kama kweli hakuna sheria zinazokuwa kinzani kwa nafasi ya Kanisa ya kutoa huduma mbalimbali nchini. “Tunaendelea kusali kwa ajili ya vituo vyetu vya kutoa malezi ya kuelekea katika huduma ya upadri na nyumba za kitawa. Naomba huko tusikanyage kanyage katika miundombinu ya hawa wanaoandaliwa kuwa mapadri. Wasipewe idadi tofauti na mwongozo wa kawaida wakaonekana wao wawe darasa la wanafunzi 25 tu, hapana. Hiyo siyo kazi ya kikund...

Baba Mtakatifu Fransisko amemteua Mhashamu Askofu Renatus Nkwande kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza

Image

Askofu R. Nkwande, ateuliwa kuwa Askofu mkuu Jimbo kuu la Mwanza

Image
Askofu Mkuu Mteule Nkwande, alipadrishwa kunako mwaka 1995. Tarehe 27 Novemba 2010, akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Bunda na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 20 Februari 2011 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam. Ana miaka miaka 7 ya Uaskofu na miaka 23 kama Padre. Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican. Baba Mtakatifu Francisko ametemua Askofu Renatus Leonard Nkwande wa Jimbo Katoliki la Bunda, kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania. Itakumbukwa kwamba, Askofu Mkuu Mteule alipadrishwa kunako mwaka 1995. Tarehe 27 Novemba 2010, akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Bunda na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 20 Februari 2011 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, utume ambao ameutekeleza kwa muda wa miaka 7 kama Askofu na miaka 23 kama Padre. Jimbo kuu la Mwanza lilikuwa wazi,...