“WAWATA HIMIZENI MIITO”
WITO umetolewa kwa wanawake wakatoliki nchini kuhimiza miito mitakatifu kuanzia ngazi za familia, jumuiya ndogo ndogo,vigango, parokia hadi majimboni ili Kanisa liweze kupata hazina kubwa ya mapadri na masista watakaolitumikia kimwili na kiroho pamoja na watu wake. Aidha imeelezwa kuwa mapadri na masista waliopo umri unazidi kuongezeka na hivyo Kanisa linahitaji vijana wa kike na kiume watakaoandaliwa katika malezi na kusomeshwa katika Seminari mbalimbali ili waweze kushika majukumu ya kichungaji na kitume katika Kanisa mahalia. Hayo yamesemwa na Katibu wa Wanawake Wakatoliki Taifa(WAWATA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa WAWATA Jimbo Kuu Dar es Salaam, Bi.Desderia Mahita wakati wa hitimisho la Kongamano la siku tatu la Kanda ya Nyanda za Juu Kusini lililofanyika jimboni Mbeya na kuwashirikisha wanawake wa majimbo 8 ya Jimbo Kuu Katolik...