Baada ya maandalizi ya kiroho kwa muda wa miaka mitatu, hatimaye, maadhimisho ya Siku ya XXXI ya Vijana Duniani kwa mwaka 2016, huko Cracovia, Poland yanayoongozwa na kauli mbiu “Heri wenye rehema maana hao watapata rehema” yamezinduliwa rasmi na Kardinali Stanislaw Dziwisz, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Cracovia nchini Poland kwa Ibada ya Misa Takatìfu. Vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia wako Poland kuzungumza lugha ya Injili, inayofumbatwa katika upendo, udugu, mshikamano na amani. Wako Jimbo kuu la Cracovia mahali alipozaliwa Mtakatifu Yohane Paulo II, Muasisi wa Siku ya Vijana Duniani, ili kufuata nyayo zake katika kutangaza na kushuhudia Injili na zawadi ya huruma ya Mungu. Hiki ni kipindi cha Sala, Tafakari ya Neno la Mungu na Sakramenti za Kanisa. Katika mahubiri yake, Kardinali Stanislaw Dziwisz amekazia kwa namna ya pekee: majadiliano na Kristo Yesu; Mahali wanapotoka; mahali walipo kwa sasa na kwamba, ni mambo yepi wanayotarajia baada ya maadhimisho ...